Halima Jumanne (20) akiwa na mwanaye mzigoni katika baa moja (jina limehifadhiwa) iliyopo Buza Kanisani jijini Dar.MSICHANA aliyejitambulisha
kwa jina la Halima Jumanne (20) amejikuta akiuza baa huku akiwa na
mtoto wa mwaka mmoja na nusu ubavuni kisa kikidaiwa hali ngumu ya
maisha.Tukio hilo la kushangaza lilijiri Juni 2, mwaka huu kwenye baa
moja (jina kapuni) iliyopo Buza Kanisani jijini Dar na kunaswa na
Opareseheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers.
Awali ilidaiwa kuwa msichana huyo alifika kwenye baa hiyo akiomba kazi ya ubaamedi huku akiwa amembeba mtoto wake huyo.
Huku akiwa amebeba mtoto, Halima akiwa kaunta kuchukua kinywaji alichoagizwa na moja ya wateja katika baa hiyo
Kwa
mujibu wa meneja wa baa hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, pamoja na
kumpokea mwanamke huyo aliyeonekana kuelemewa na msongo wa mawazo,
alimshauri aachane na ubaamedi na kutafuta kazi nyingine zinazoweza
kumuingizia kipato kama vile za ndani ambapo msichana huyo alijibu yupo
tayari ikiwa atapata.
Waandishi
wetu walipopata taarifa ya kuwepo kwa baamedi huyo, walifika kwenye baa
hiyo na kumshuhudia msichana huyo akihudumia wateja na mtoto huyo akiwa
ananing’inia ubavuni.
Akizungumza na OFM, Halima alisema yeye ni mwenyeji wa Kigoma na aliingia jijini Dar kutokana na matatizo mengi yaliyopo huko ikiwa ni pamoja na kufariki dunia kwa mama yake ambaye alikuwa akimtegemea kwa kila kitu.
Akizungumza na OFM, Halima alisema yeye ni mwenyeji wa Kigoma na aliingia jijini Dar kutokana na matatizo mengi yaliyopo huko ikiwa ni pamoja na kufariki dunia kwa mama yake ambaye alikuwa akimtegemea kwa kila kitu.
Halima alisema, Dar alifikia Kongowe, Temeke kwa mwanaume aliyemtaja kwa jina la Michael na ndiye aliyezaa naye mtoto huyo.
“Kwa
kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele yule mwanaume alibadilika tabia
na kuanza kunipiga kutwa kucha bila kunipa hela ya matumizi.
“Ilifika
hatua nikawa nakwenda kubeba mchanga kutoka bonde la Mto Mzinga na
kuuza ili nipate hela ya kununulia chakula, hapo ni siku saba tu tangu
nijifungue.
“Kutokana
na mateso hayo, nilimtafuta kaka yangu ambaye alinichukua na kuishi
kwake Buza ambapo huko nako niliishi kwa kuambulia kipigo mfululizo
kutoka kwa wifi yangu.
“Nilimwambia kaka kuhusiana na mateso hayo lakini alishindwa kusuluhisha jambo lililonifanya kulifikisha suala hilo kwenye serikali ya mtaa.
“Nilimwambia kaka kuhusiana na mateso hayo lakini alishindwa kusuluhisha jambo lililonifanya kulifikisha suala hilo kwenye serikali ya mtaa.
“Viongozi
wa mtaa waliamua kunipa hifadhi ya malazi kwenye nyumba ya mjumbe
mmoja wa mtaa huku kesi ikiendelea kusikilizwa,” alisema Halima.
Huku
akionesha makovu na uvimbe jichoni yaliyotokana na kipigo, msichana
huyo alisema kutokana na hali ya maisha kuwa magumu aliamua kufanya kazi
ya u-mama ntilie wa kuuza chipsi mpaka usiku wa manane akiwa na mwanaye
mgongoni.
“Kaka
zangu sijui nifanyeje? Sina msaada wowote ndiyo maana niliamua kuja
hapa baa nifanye kazi za hapa angalau nipate hela ya kula na mwanangu.
Wamenishauri nitafute kazi nyingine, lakini mimi sijasoma, naomba kama
kuna mtu anisaidie nipate kazi nitafanya vizuri tu,” aliomba Halima.
No comments:
Post a Comment