Pages

May 27, 2014

WAZIRI WA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAZI AFANYA ZIARA WILAYANI MVOMERO


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anna Tibaijuka akipata maelezo ya jiwe la alama ya mpaka (beacon) unaotenganisha vijiji vya Dihombo na Mkindo wilayani Mvomero kabla ya kukabidhi hatimiliki za kimila jana. Hatua ya kutolewa hati ni baada ya kazi ya kupanga matumizi ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji na hatimaye kumaliza mgogoro uliokuwepo awali. Anayetoa maelezo ni Mpima Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi Bw. Musa Stephen.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anna Tibaijuka akishiriki kusoma ramani za mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji cha Lukenge Wilayani Mvomero uliopangwa na wanakijiji wenyewe.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anna Tibaijuka akizungumza na mmoja wa wafugaji wa kijiji cha Lukenge Mvomero kabla ya kukabidhi hatimiliki za kimila.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anna Tibaijuka akizungumza na kundi la wafugaji wa kijiji cha Lukenge Mvomero kabla ya kuwakabidhi hatimiliki za kimila.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anna Tibaijuka akikabidhi hatimiliki za kimila kwa mmoja wa wakulima Bw. Edward Cornrad Joseph kwa niaba ya mwanae Conrad Edward katika kijiji cha Lukenge Mvomero baada ya kupangwa kwa matumizi ya ardhi na kumalizika kwa mgogoro uliokuwepo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anna Tibaijuka akikabidhi hatimiliki za kimila kwa mmoja wa wafugaji Bw. Ramadhani Njakuri Maitei katika kijiji cha Lukenge Mvomero baada ya kupangwa kwa matumizi ya ardhi na kumalizika kwa mgogoro uliokuwepo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anna Tibaijuka akikabidhi hatimiliki za kimila kwa mmoja wa wakulima Bibi Devota Elias Mavika kijiji cha Lukenge Mvomero baada ya kupangwa kwa matumizi ya ardhi na kumalizika kwa mgogoro uliokuwepo.Picha zote na Rehema Isango wa Wizara ya Ardhi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...