Mmoja wa watuhumiwa hao akipakiwa kwenye Gari la Polisi tayari kwa Kupelekwa Mahakamani kusikiliza kesi yao.
WATU 17
wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu Mkazi jijini Arusha,
kujibu mashitaka 16 yakiwemo ya kuua kwa kutumia bomu,kutesa binadamu na
kusajili vijana na kuwapeleka nje ya nchi kufanya ugaidi.
Watu hao
walifikishwa mahakamani hapo leo na kusomemewa shitaka hilo mbele ya
Hakimu Mkazi Mustafa Siama ambapo hawakutakiwa kujibu chochote kutokana
na kile kilichoelezwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi
hiyo.
Watuhumiwa
hao wanadaiwa kutenda tukio hilo Aprili 13,katika nyumba ya kulala
wageni na baa ya Arusha Night Park iliyopo Mianzini jijini hapa,ambapo
kesi hiyo imeahirishwa hadi juni 11 mwaka huu kwa mtuhumiwa namba moja
na namba nne na watuhumiwa wengine waliobaki kesi yao itatajwa tena juni
12
Katika
tukio hilo la mlipuko huo wa bomu watu 14 walijeruhiwa vibaya katika
maeneo mbalimbali ya miili yao hali iliyopelekea mmoja wa majeruhi hao
aliyefahamika kwa jina la Sudi Ramadhani mkazi wa Kaloleni jijini hapa
kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa
Arusha ya Mount Meru.
Akizungumza
na waandishi wa habari Makao Makuu ya Polisi Arusha,kabla ya watuhumiwa
hao kufikishwa mahakamani,Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai nchini (DCI)
Isaya Mngulu amesema kuwa mara tu baada ya kutokea kwa tukio hilo,
polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama walianza
upelelezi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao.
Ameongeza
kuwa pia siku hiyo hiyo ya tukio hilo la mlipuko wa bomu katika baa ya
Arusha Night Park muda mfupi baadae bomu lingine la aina ileile
liligundulika kutegwa katika baa ya Washington ya jijini hapa ambapo
bomu hilo liliondolewa katika eneo hilo bila kuleta madhara .
"Aidha
baadhi ya watuhumiwa hawa pia walibainika kuwa na mikakati ya
mashambulizaya namna hiikatika maeneo mengine na sehemu mbalimbali hapa
nchini ambazo ni taasisi za Serikali na sehemu zenye mikusanyiko ya
watu,ambapo pia wanajihusisha na uandaaji wa vijana kutoka mikoa
mbalimbali hapa nchini na kuwapeleka nchi za nje ili kujiunga na makundi
ya kiuhalifu"alisema Mkurugenzi huyo wa Mashitaka nchini.
Mkurugenzi
huyo amesema kwamba upelelezi wa matukio haya bado unaendelea ili
kuwakamata watiliwa shaka wenginewaliobaki katika matukio ya milipuko ya
mabomu katika Kanisa Katoliki Olasiti uwanja wa Soweto yaliyotokea
mwaka jana jijini hapa na sehemu nyingine nchini.
CHANZO MTAA KWA MTAA
No comments:
Post a Comment