Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo, kushoto ni Mkurugenzi wa kituo cha Maendeleo na Utamaduni, Anthony Mhando.
Na Lilian Lucas, Morogoro.
Watu kadhaa akiwemo mwandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Juma Mtanda ametunukiwa tuzo ya heshima ya Uluguru Award ya mwaka 2013/14, kuhusu uandishi wa habari na upigaji picha za matukio mbalimbali yanayogusa jamii, mkoani Morogoro.
Tuzo hiyo imetolewa na Kituo cha Maendeleo ya Utamaduni cha mjini Morogoro (Kimau).
Akitangaza tuzo zilizotunukiwa kwa taasisi mbalimbali, Mkurugenzi wa kituo hicho, Morogoro Anthony Mhando, alisema lengo ni kuchochea uajibikaji kwa kufuata misingi ya utawala bora katika nyanja mbalimbali.
Mhando alizitaja nyanja hizo kuwa ni pamoja na uandishi wa habari zinazogusa jamii, ujasiriamali, uwekezaji, utawala bora, michezo na usanii.
Mhando aliwataja washindi wa tuzo hizo kuwa ni pamoja na mpigapicha wa gazeti la mwananchi mkoa wa Morogoro, Juma Mtanda aliyetwaa tuzo hizo kutokana na mchango katika kuripoti baadhi ya habari za migogoro ya wakulima na wafugaji, mafuriko yaliyowakumba wananchi wa la kijiji cha Magole yaliyotokea hivi karibuni.
Wengini waliotwaa tuzo ya uandishi wa habari ni Mwandishi Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha ITV ambaye ni Mwenyekiti wa Morogoro Press Club, Idda Mushi, John Nditi kutoka TSN na Walda Magongwa wa kituo cha redio cha Planet FM.
Kwa upande wa viongozi utawala bora ni mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood, mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera huku ngazi ya wajasiliamali, Bacho Sadik Bacho ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo (TCCIA) akitwaa tuzo hiyo. Alisema Mhando.
Kwa upande wa taasisi za kifedha CRDB yenyewe iliibuka na tuzo ya taasisi bora ya kifedha huku kampuni ya uwekezaji kiwanda cha kusindika tumbaku (TLTC) wakitwaa tuzo ya kampuni bora wakati kwa upande wa michezo, jina la Shomari Kapombe likiibuka katika soka, Cosmas Cheka ambaye ni mwanamasumbwi, Azack Sokas aliyetwaa tuzo kupitia mchezo wa kareti.
Viongozi wa michezo ni Zumo Makame, Awadh Komba na Paschol Kianga ambaye ni mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) kwa wasanii Miss Tanzania 2013 Happness Watimanya na Afande Sele anayejisghuhulisha na muziki wa kizazi kipya huku mkuu wa mkoa wa Morogoro akiwa mgeni rasmi katika haflas hiyo iliyofanyika ukumbi wa Mambo Club.
No comments:
Post a Comment