Pages

April 13, 2014

MAUAJI YA WAKULIMA YAENDELEA HUKO KITETO, POLISI YATOA TAMKO



 
Picha na maktaba
 

Mkulima Kiteto auawa kwa kuchinjwa * 
 Kamati ya usalama yaketi kwa dharura * CCM yalaani yatoa tamko

NA. MOHAMED HAMAD

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Masudi mkulima (mgogo) mkazi wa kitongoji cha Orkeri Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, ameuawa kwa kukatwa kwa kitu chenye ncha kali shingoni (kuchinjwa) na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafugaji wanaovamia makazi ya wakulima
Tukio hilo limetokea April 3 mwaka huu baada ya baadhi ya jamii ya kifugaji (wamasai) kuvamia wakulima kwa kuwapiga kisha kuwachomea makazi yao ili waweze kuondoka na kuyaacha maeneo yao ambayo yatatumika kwa shughuli za ufugaji

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara ambae pia ni Kamishna mwandamizi wa wa Polisi (SACP) Deusdedit Nsimeki amesema kuwa matukio ya mauaji Kiteto yamekuwa yakijitokeza kutokana na jamii za wakulima na wafugaji kugombea ardhi "Huwezi kuamini mwandishi suala hili linaonekana kuwa na mvuto mkubwa Wilayani hapa kwani baadhi ya Viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wana Siasa wanadaiwa kunufaika na migogoro hiyo kwa namna moja ama nyingine"
"Jeshi la Polisi tumejipanga hatutamwonea mtu, sheria itafuata mkondo wake awe mwanasiasa au kiongozi yotote wa Serikali atakaye husika tutamkamata na kumfikisha mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake"alisema Kamanda Nsimeki

Alisema wapo wanasiasa ambao kwa namna moja ama nyingine wameonekana kujitokeza katika mgogoro huu, wakiwemo baadhi ya viongozi wa Halamshauri na kusababisha mgogoro kuendelea

Kamanda Nsimeki alisema hakuna mtu anayeshikiliwa kwa mauaji hayo na kwamba Jeshi la Polisi kiteto likiongozwa na Mkuu wa Polisi Mrakibu Mwandamizi Evaristi Chuwa watahakikisha waliohusika na mauaji hayo wanakamatwa na kufikishwa mahakamani

Kutokana na tukio hilo kamati ya Ulinzin na usalama imeketi katika kikao cha dharura mbapo pamoja na mambo mengine imelaani mauaji hayo na kusema jitihada zitafanyi kakabiliana na mauaji hayo

KAMATI YA SIASA
Chama cha mapinduzi CCM Wilayani Kiteto kimelaani mauaji ya kinyama yaliyofanywa na baadhi ya wananchi wanaodaiwa kuwa wanatokana na jamii ya kifugaji wamasai na kuiagiza Serikali kutokomeza vitendo vya mauaji vinavyojitokeza kila mara
Akizungumza hayo Abeid Maila mara baada ya kwenda kushuhudia mwili wa marehemu uliopo katika Hospitali ya wilaya ya Kiteto alisema, huo ni uhalifu ambao Serikali ya Chama cha Mapinduzi CCM haiwezi kuvumilia
Maila ameitaka kamati ya Ulinzi na usalama Kiteto kuhakikisha inavikomesha vitendo vya mauaji ya mara kwa mara vinavyoendelea kujitokeza na kusababisha wananchi kukosa imani na Serikali yao ambayo kqwa sasa nndio iko madarakani
"Sisi Chama tumechukizwa na kitendo hiki tumekutana kamati ya siasa kushuhudia mwili wa ndugu yetu ambaye amekatishwa maisha yake kwa maksudi, na vitendo hivi vinatisha sana iko haja kwa Serikakali tunayoiongoza kufanya kazihii kwa makini natupate taarifa"

"Waziri Mkuu Miizengo Pinda alipofika hapa alituliza munkari wa wananchi kwa kuiagiza Serikali kufanya mambo mbalimbali yakiwemo kutenga maeneo ya kilimo na mifugo lakini toka aondoke kazi hiyo haijafanyika"
Kwa mujibu wa Katibu huyo wa CCM alisema Waziri Mkuu pamoja na mambo mengine baada ya kuwasili Kiteto kutokana na mauaji ya zaidi ya watu 16 mapemamwakahuu aliitaka Serikakli ya Kiteto kuhakikisha amani inarejeshwa kwa kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji
Pia alisema ili kuondoa tofauti ya mkulima na mfugaji maeneo ya kilimo na mifugo yawekewe mipaka ambayo itasaidia pande hizo kutoingiliana kwa shughuli za kiuchumi ambazo zinafanywa na wenyeji hao

WANANCHI 

Baadhi ya wananchi wamesema kifo cha mkulima huyo ni mwendelezo wa mauaji yanayofanywa na watu wa jamii ya kifugaji baadhi ya wamasai ambao inadaiwa chanzo ni Halmshauri ya Wilaya kuwagawa wananchi kwa itikadi ya kikabila
Akizungumza hayo Luka Ngidi (30) majeruhi aliyelazwa kwa kujeruhiwa na wafugaji akiiwa shambani kwake baada ya kutembelewa na kamati hiyo ya siasa ya Wilaya amesema Serikali ya Kiteto iko likizo na ndio maana kila kukicha mauaji hayaishi huku viongozi wakibakia kushiriki mazishi

" Naweza kusema mimi nilikwisha kufa tu, maana nilizingirwa na wamasai shambani kwangu baada ya ngombe kuingizwa kwa nguvu, nilipigwa fimbo nyingi sana nawashukurui madaktari sana wameokoa maisha yangu"

Serikali hii iko likizo hapa hatuna Mbunge wala Mkuu wa Wilaya tunaishi kama hatuna Serikali nawaomba kwakuwa ninyi ndio mmeweka hii Serikali madarakani wasimamieni hawa viongozi tukifa wataongoza akina nani alisenma kwa machungu majeruhi huyo

Kwa upande wake Dkt Thomas Ndalio akieleza hakli ya mgonjwa huyo alisema kwa sasa a naendelea vizuri baada ya kupata matibabu, akisisitiza kuwa hali yake ilikuwa mbaya na sasa anaweza hata kuongea vizuri na hata kula

Kuhusu marehemu huyo alisema amekatwa nma kitu chene ncha kali shingoni kasha kuchomwa na mkuki hali iliyompelekea kifo hicho ambacho kimevuta hisia za watu wengi wilayani kiteto akisisitiza kuwa mauaji hayo yataisha endapo Serikali iitaamua kukabiliana nayo ipasavyo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...