Pages

April 6, 2014

Maneno ya Albert Msando juu ya Bunge la Katiba.

msandoWakili wa Kujitegemea ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mabogini wilaya ya Moshi vijijini Albert Msando ametoa ya moyoni kwa kile kinachoendelea kupitia Bunge la Katiba kwenye Exclusive interview namillardayo.com.
Ameanza kwa kusema>>’Nachokiona kwenye Bunge la Katiba ni maslahi binafsi niseme tu bila kusita kwamba maslahi binafsi,binafsi inaweza kuwa ya mtu binafsi yeye kama yeye na pia kama chama au makundi,mpaka sasa hivi hatujaweza kuwa na bunge la katiba ambalo linajitambua kwamba pale ni kwa Watanzania wawakilishi wa Wananchi’
‘Bado kila mtu anachukua nafasi yake au utambulisho wake uliompeleka bungeni kwa hiyo kama mimi nimekuja kwa ajili ya wafugaji nataka katiba ielekee kwenye ufugaji,kama nimekuja kwa ajili ya chama cha siasa basi chama cha siasa kwa ajili ya kushika dola kwa hiyo unakuta ubinafsi umekua mwingi’
‘Kuna watu wanafikiria 2015 kuwasaidia kuingia kwenye nafasi za uongozi sasa hilo ni tatizo na inasikitisha sana kwamba mpaka sasa hivi hatujaweza kuona umoja ndani ya bunge la katiba ambao tungeutaka ili waweze kujadili mambo ya msingi ya mustakabali wa nchi kuliko sasa hivi wanavyoangalia yale wanayotaka wao kufanikisha’
‘Muda ni kikwazo kwa sababu na sisi tumelipeleka hili jambo kwa haraka kwamba kwa vyama vya upinzani wenyewe walikua wanaona kulazimisha katiba mpya ni ushindi kwa wananchi kwamba kutakua na katiba mpya ambayo itatoa nafasi labda ya uchaguzi huru na haki katika demokrasia’
‘Serikali ya Ccm yenyewe ikaona ni ushindi kwamba sasa wanaweza kuweka kama historia kwamba sisi ndiyo tuliowezesha katiba mpya kupatikana,kutokana na haraka hizo tumejikuta hili zoezi tunataka likamilike ndani ya muda mfupi,matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona sasa hivi’
‘Tunahitaji muda zaidi wananchi wanahitaji muda kuelewa kwa sababu katiba sio kitu cha siku moja au siku mbili ni jambo linalotakiwa kutuongoza kwa miaka 100 au 200 ijayo,nchi kama Marekani imekua na katiba za ma-miaka na miaka,sisi tusitengeneze katiba baada ya miaka 50 tunataka katiba nygingine maana hiyo ndiyo tabia yetu Watanzania’.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...