Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete (aliyenyoosha mkono), akimuonyesha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana mandahari ya eneo la Ziwa Tanganyika, linalotumiwa na wavuvi katika eneo la Kabwe wilayani Nkasi mkoani humo, Kinana alipokuwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia ya kuzitatua katika eneo hilo la Wavuvi.
Mfanyabiashara ya kusafirisha na kusindika samaki kutoka ziwa Tanganyika, Mohamed Shibibi (wapili kushoto) akimpatia maelezo Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana jinsi anavyohifadhi samaki katika majokofu baada ya kuvuliwa, Kinana alipokagua shughuli za mfanyabiashara huyo, kwenye eneo la wavuvi wa Kata ya Kabwe, wilayani Kansi mkoani Rukwa. Kushoto ni Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume.
Kinana akitazama lundo la samaki aina ya migebuka kwenye kituo cha wavuvi cha Kabwe, katika ziwa Tanganyika
Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume, akihutubia wananchi katika mkutano wa Kinana, uliofanyika kwenye Ofisi ya CCM Kata ya Kabwe .
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Makao Makuu ya CCM, Godfrey Chongolo, akiwa na kina mama waliokuwa wakikunja samaki aina ya migebuka katika mwambao wa ziwa Tanganyika eneo la Kabwe, Wilayani Nkasi mkoani Rukwa.
No comments:
Post a Comment