Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal Shelutete akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha |
Taifa ya Katavi kuwa inatarajiwa kukabidhiwa kwa wawekezaji kutoka nchini
Afrika Kusini ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe....
Lazaro Nyalandu.
Shirika la Hifadhi za Taifa linalosimamia Hifadhi ya Taifa ya Katavi pamoja
na Hifadhi nyingine 15 nchi nzima linapenda kukanusha habari hiyo iliyoandikwa
kwa lengo la kupotosha umma kama ifuatavyo.
Mosi, hakuna mpango wala uamuzi wowote uliopo au uliokwisha kufanywa wa
kuingia Mkataba
wa Uendeshaji wa aina yoyote ile baina ya Shirika la Hifadhi za Taifa na
Mwekezaji yeyote kutoka nchini Afrika ya Kusini ikiwa ni pamoja na
African Parks Network waliotajwa katika habari husika.
Pili, Sheria inayosimamia uanzishwaji wa maeneo ya Hifadhi za Taifa ikiwemo
Katavi imelipa dhamana hii pekee shirika kusimamia maeneo haya kwa niaba ya
Watanzania na ni kinyume cha sheria kukabidhi kwa wawekezaji kwa ajili ya
usimamizi kama ilivyobainishwa katika habari hiyo.
Tatu, Shirika la Hifadhi za Taifa bado linao uwezo thabiti wa kusimamia
uendeshaji wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi ili kuhakikisha rasilimali za wanyama
na mimea zinaendelea kutunzwa kwa miaka mingi ijayo kama ambavyo imekuwa
ikifanya tangu kuanzishwa kwa hifadhi hiyo mwaka 1974.
Aidha, kama ambavyo shirika limekuwa likipanga katika mipango yake ya
maendeleo mwaka hadi mwaka, katika mwaka mpya wa fedha ujao shirika limepanga
kuongeza idadi ya watalii katika Hifadhi za Kusini ikiwemo Katavi,Saadani,Mikumi na Ruaha.
Mkakati huu utahusisha
kuongeza ubora wa utoaji huduma ikiwa ni pamoja na malazi ili kukuza utalii wa
ndani. Shirika litafungua ofisi Jijini Dar es Salaam na kuimarisha ofisi za
Mwanza na Iringa ili watalii wapate taarifa za Hifadhi na kuweza kufanya
‘bookings’ kwa urahisi. Aidha, kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa masoko ya
nje, Shirika sasa litaanzisha ‘Road shows’ mbalimbali kwa soko la ndani na nchi
za jirani. Vilevile, Shirika litaongeza kujitangaza kupitia Mitandao ya Jamii,
TV, majarida na tovuti ya Shirika itaboreshwa katika kuarifu wadau masuala
mbalimbali yanayojiri kwenye Hifadhi zetu.
Tayari Shirika limeanzisha Kurugenzi mpya ya Utalii na Masoko kwa ajili ya
kutekeleza mkakati huu wa kuzifanya hifadhi za ukanda wa kusini kuvutia watalii
wengi zaidi.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
30.03.2014
No comments:
Post a Comment