Pages

March 17, 2014

MAKAMU WA RAIS DK BILAL AFUNGUA MKUTANO WA WAWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA ISRAEL JIJINI DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipongezwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, baada ya kufungua rasmi mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014. Kulia ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi (wa pili kulia) na Mwakilishi wa Ubalozi wa Israel kwa nchi za Tanzania, Kenya Uganda na Seychells, Gilad Millo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Kampuni ya Balton Tanzania, baada ya kufungua rasmi mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014. Kushoto ni Mtaalamu wa Kilimo, Maximillian Sarakikya (kulia) ni Mkuu wa Maendeleo ya Biashara na Habari, Linda Byaba
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwahutubia ukumbini humo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na Makamu  Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Phillip Mangula, ambaye pia alikuwa ni miongoni mwa washiriki wa mkutano huo, mara baada ya kufungua mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...