Pages

February 16, 2014

JK ATUA MJINI DODOMA KUONGOZA KIKAO CHA NEC

 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma tayari kuongoza kikao cha NEC .
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Dodoma mara tu alipowasili kwenye uwanja wa ndege mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia ngoma ya asili kutoka kikundi cha ngoma cha mkoa wa Dodoma wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya mrisho Kikwete akiongoza kikao cha NEC mjini Dodoma na kuwaambia wana CCM kuwa uvumilivu una ukomo wake hivyo waache unyonge.
Baadhi ya Wajumbe wa NEC wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kikao cha NEC kilichoanza jioni ya jana mjini Dodoma .
 Mjumbe wa NEC Ndugu Bernard Membe akijadiliana jambo ndani ya ukumbi wa NEC na Martine Shigela kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC mjini Dodoma.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro pamoja na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakhia Hamdani Meghji wakipitia makablasha kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC mjini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara) Ndugu Mwigulu Lameck Nchemba akijadiliana jambo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...