Shule moja ya sekondari ya
wasichana iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, imelalamikiwa na wanafunzi
pamoja na wazazi kuwa mabinti wanajihusisha na vitendo vya ngono vya jinsia moja
(usagaji).
Akizungumza na NIPASHE mmoja wa wazazi (jina linahifadhiwa)
alisema shule hiyo imepoteza sifa kwa kuwa kuna wimbi kubwa la wanafunzi
wanaojihusisha na vitendo hivyo vya usagaji.
Alisema mtoto wake alikuwa
ameanza kidato cha kwanza mwaka jana na baada ya kumuandikisha ndipo baadhi ya
watu walipomueleza kuwa shule hiyo kwa sasa ina sifa mbaya ya mchezo ‘huo
mchafu.’
"Baada ya kuelezwa nikasema nitalifanyia kazi jambo hilo hivi
karibuni katika kupekua madaftari ya mwanangu nakutana na kibarua cha mapenzi
alichoandikiwa na msichana mwenzake niliumia sana na nilitumia nguvu kumbana
bila hivyo asingeniambia," alisema
Alisema ilimbidi amhamishe binti yake
na kujiunga na shule moja ya sekondari iliyopo mkoani Tanga kwa ajili ya
kuendelea na masomo ya kidato cha pili mwaka huu.
Mzazi huyo alisema
anashangazwa ni kwa nini hatua hazichukuliwi wakati suala hilo ni la hatari
kwani watoto wao wataharibika kiakili pamoja na kimwili na wanaweza kuambukizana
VVU na Ukimwi..
Alisema wakati mwanaye akisoma katika shule hiyo alikuwa
akihudhuria vikao vya wazazi mara kwa mara na kwamba kila kikao walikuwa
wakifukuzwa wanafunzi kutokana na mwenendo huo.
"Hili tatizo ni kubwa na
kufukuzwa kwa mwanafunzi sidhani kuwa wanatatua tatizo nadhani hakuna usimamizi
mzuri kwani wangeweza kudhibiti kwa haraka tatizo hilo kabla ya kuwa kubwa,"
alisema
Pia alisema ndugu yake imembidi amhamishe mwanae na kumtafutia
shule nyingine kwa kuhofia binti yake kurubuniwa kwani wanakuwa ni wadogo na
hawaelewi chochote, hivyo inaweza kuwa rahisi kudanganywa na kuingia kwenye
vitendo hivyo viovu.
Alisema kuwa hata kiwango cha ufaulu kwa sasa shule
hiyo imeshuka kutokana na tatizo hilo kwa wanafunzi .
Hata hivyo, NIPASHE
ilizungumza na mwanafunzi mmoja ambaye anasoma katika shule hiyo kuhusiana na
suala hilo ambapo alikiri kuwepo kwa jambo hilo na kueleza kuwa wanaofanya
mchezo huo ni wa kidato cha tano na cha sita.
"Mimi hawajanifanyia ila
najua wanaofanya mchezo huo ni wale walioko kidato cha tano na cha sita,"
alisema Pia kuna baadhi ya wazazi wengine wamekuwa wakilalamikia jambo hilo na
kueleza kuwa ndugu zao imewalazimu kuwahamisha watoto wao kutokana na vitendo
hivyo vinavyofanyika shuleni hapo.
Chanzo:Nipashe
Post a Comment