Rais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati akimtangaza Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho hilo,ambaye
ni Selestin Mwesigwa (aliewahi kuwa katibu mkuu wa Yanga) (wa pili kushoto)
pamoja na Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya
Kisheria ya TFF,Wakili Evodius Mtawala
(kulia) wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana.Kushoto ni Afisa Habari wa TFF,Boniface
Wambura.
Rais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (katikati) akimkabidhi Mkurugenzi wa Vyama na
Masuala ya Kisheria,Wakili Evodius Mtawala nakala ya ilani yake ya uchaguzi
wakati akimtambulisha kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.kushoto ni
Katibu Mkuu wa Mpya wa TFF,Selestin Mwesigwa.
Rais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu wa TFF, Selestin
Mwesigwa nakala ya ilani yake ya uchaguzi wakati akimtambulisha kwa waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam.
SHIRIKISHO la soka
Tanzania, TFF limemuajiri Katibu Mkuu wa zamani wa Timu ya Yanga, Selestin
Mwesigwa kuwa katibu mkuu mpya wa shirikisho hilo.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
imesema kuwa, Mwesigwa alizaliwa mwaka 1970, ana digrii ya masuala ya kimataifa
kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam na diploma ya mafunzo ya
sheria.
Malinzi aliongeza kuwa
Mwesigwa amefanya kozi kadhaa za masuala ya utawala ndani na nje ya nchi
zikiwemo kozi za utawala wa mpira zilizotolewa na
FIFA.
Rais huyo alisema Ajira
yake ya mwisho ya Mwesigwa ilikuwa Ukatibu mkuu wa klabu ya Yanga ya Dar es
salaam, hivyo ana uzoefu mkubwa wa masuala ya uongozi ikizingatiwa amefanya kazi
katika mashirika mbalimbali ikiwemo Plan
International.
Aidha, Malinzi alisisitiza
kuwa Mwesigwa alipokuwa katibu mkuu wa Yanga alishiriki kikamilifu katika
mchakato wa kuanzisha Bodi ya Ligi kuu na ule wa Yanga kuingia udhamini na
kampuni ya bia ya TBL, hivyo amekidhi vigezo vya kushika wadhifa huo mkubwa
ndani ya TFF.
TFF pia imemuajiri katibu
wa Simba SC, Wakili Evodius Mtawala kuwa Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya
Kisheria ya TFF.
Rais Malinzi alisema
Mtawala ana Shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shahada ya
Uzamili ya uongozi wa Biashara ya Chuo Kikuu cha
ESAMI.
Rais aliongeza kuwa
Mtawala ambaye ajira yake ya mwisho ilikuwa Ukatibu mkuu wa Simba Sc , Klabu
mwanachama wa TFF, ana uzoefu ambao utasaidia sana kukabili changamoto
mbalimbali za vyama wanachama wa TFF.
Aidha Rais alisema uzoefu
wake na ujuzi wa masuala ya sheria utasaidia kutatua masuala mbalimbali ya
kisheria na kikatiba ndani ya shirikisho hilo.
Nafasi ya Mkurugenzi wa
Mashindano wa TFF imeachwa wazi kufuatia waombaji wote walioomba wa ndani na nje
ya nchi kutokidhi vigezo, hivyo kamati ya utendaji imeagiza nafasi hii itangazwe
upya na wale walioomba mara ya kwanza wasiombe tena.
Rais Malinzi alisema Bwana
Idd Mshangama atakaimu nafasi hii kwa sasa mpaka mtu mwingine
atakapopatikana.
Pia nafasi ya Mkurugenzi wa
ufundi imebaki wazi baada ya waombaji wote kutokidhi vigezo, hivyo Bwana Salum
Madadi atakaimu nafasi hiyo na Rais Malinzi ameagiza itangazwe tena na walioomba
wasiombe tena.
Nafasi nyingine iliyobaki
wazi ni Mkurugenzi wa fedha na utawala, hivyo itatangazwa tena na kwasasa Bwana
Danny Msangi atakaimu.
Afisa habari wa TFF
ataendelea kuwa Bwana Boniface Wambura Mgoyo.
Rais Malinzi alisema ajira
zote zitaanza rasmi januari Mosi mwakani na anawatakia kazi njema, huku akiwa na
imani kubwa kuwa watasukuma mbele gurudumu la maendeleo ya mpira wa
miguu.
Katika hatua nyingine, TFF
imeteua wajumbe wa kamati ya uchaguzi na kamati ya Rufani ya Uchaguzi na kamati
ya soka la ufukweni.
Kamati ya uchaguzi inaundwa
na Mwenyekiti, Wakili Melchesedek Lutema, Makamu wake, Wakili Walter Chipeta na
Wajumbe Hamidu Mahmoud Omar, Jeremiah John Wambura na Hassan
Dalali.
Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi
ya TFF itakuwa chini ya Mwenyekiti , Wakili Julius Lugaziya, Makamu wake,
Wakili Mwita Mwaisaka na Wajumbe Juma Abeid Khamis, Rashid Dilunga na Masoud
Issangu.
Na kamati ya Soka la
Ufukweni itakuwa chini ya Mwenyekiti Ahmed Mgoyi, makamu mwenyekiti, Shafii
Dauda na Wajumbe Deo Lucas, Juma Mgunda, Boniphace Pawasa,

Post a Comment