Hii ni moja kati ya stori kubwa za Kenya nilizozipata hivi karibuni, japo nimechelewa kuiweka hapa kutokana na millardayo.com kuchelewa kurudi kwenye utaratibu wake wa kawaida… ni moja ya headlines kubwa nilizopenda na watu wangu wajue.
Mtandao wa Jambo umeripoti kwamba baadhi ya Makatibu wakuu wa Wizara na wajumbe wa kamati mbalimbali za katiba nchini Kenya, wamekiuka mpango wa Serikali kupunguza matumizi kwa kununua magari ya kifahari yakiwemo ya aina ya Limosine jambo ambalo limefanya Hazina kuwapa Onyo zito.
Taifa la Kenya lilipata taarifa kwamba viongozi kadhaa wa juu wamenunua magari 30 aina ya Mercedez Benz ndani ya mwezi mmoja ambapo wengine wamedaiwa kujichukulia magari ya ulinzi kinyume na taratibu.
Unaambiwa katibu mkuu wa Hazina Henry Rotich jumapili iliyopita aliliambia gazeti la The Daily Nation kwamba taifa halitavumilia matumizi ya anasa na ufisadi ambapo Wizara yake haijapitisha matumizi ya magari ya kifahari.
No comments:
Post a Comment