Prince William na Mkewe |
London
Katika taarifa ya
Kasri la kifalme la Kensington, Duchess wa Cambridge amepata mtoto wake wa
kwanza majira ya saa kumi na dakika ishirini na nne za jioni kwa saa
Uingereza,akiwa amezaliwa na kilo 3.62874.
Taarifa zinazohusiana
Kasri la Kifalme
limesema, mama na mwanawe wanaendelea vyema na watasalia hospitalini usiku huu.
Baba wa Mtoto, Prince
William alishuhudia wakati mtoto akizaliwa.
Tangazo la kuzaliwa
kwa mtoto limetolewa na kuonyeshwa mbele ya lango kuu la Kasri kuu la kifalme
la Uingereza la Buckingham kama utamaduni na mila za Uingereza zilivyo.
Taarifa rasmi
iliyosainiwa na jopo la madaktari bingwa kuthibitisha kujifungua kwa Duchess wa
Cambridge ilipelekwa kwenye kasri la kifalme chini ya ulinzi wa polisi.
Malkia wa
Uingereza,Duke wa Edinburgh,Prince wa Wales, Duchess wa Cornwall na Prince
Harry pamoja na wanandugu wa familia zote wametaarifiwa juu ya kujifungua
salama kwa Kate na wote wamepokea vizuri habari hii, Imesema taarifa hiyo ya
Kasri la kifalme.
Waziri Mkuu wa
Uingereza, David Cameron ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ujumbe
wa kuwapongeza Prince William na mkewe kwa kupata mtoto wa kiume na kusema nchi
nzima itashangilia kwa ujio wa mtoto wa kiume.
Kiongozi wa chama cha
Labour Ed Miliband pia ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter
"pongezi nyingi kwa Duke na Duchess wa Cambridge. Nawatakia wao na mtoto
wao furaha na afya njema."
No comments:
Post a Comment