Mkurugenzi wa Kampuni ya A.E.Building and Civil Enginering Limited ya Arusha,Ally Swai akizungumza na waandishi wa habari. |
Mafundi wakiendelea na ujenzi
Arusha.
Wananchi wa
Kata ya Lemara,jijini Arusha wataondokana na kero iliyokua ikiwasumbua
kwa muda mrefu hasa wakati wa mvua baada ya daraja jipya la Kikwakwaru B
linalojengwa kwa gharama za Mfuko wa barabara kukamilika mwezi huu.
Akizungumzia maendeleo ya ujenzi huo,Mhandisi wa Jiji
la Arusha, Elias Biromo alisema ujenzi umekamilika kwa asilimia 60 na
linajengwa kwa kiwango walichokubalina na kampuni ya ujenzi ya A.E.Building and
Civil Enginering Limited ya Arusha kwa gharama ya Sh 157 milioni.
Amesema daraja hilo litakua ni ukombozi kwa wananchi wa
Kata hiyo na Kata jirani ambao wamekua wakipata shida kutumia daraja ambalo
lilikua haliwezi kuhimili idadi ya magari na kuwa mpango ni kuunganisha
barabara hiyo kutoka Njiro hadi Kata ya Sombetini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni inayojenga daraja
hilo,Ally Swai amesema ujenzi ulichelewa kutokana na mvua zilizosimamisha
ujenzi kwa muda na upungufu wa vitendea kazi ambayo ilikua ni changamoto
katika kazi hiyo.
“Nawataka wananchi wavumilie ujenzi wa daraja unahitaji
umakini mkubwa na utakamilika muda si mrefu,kumekua na maneno ya kisiasa ambayo
lengo lake sio zuri jambo la msingi ni daraja likamilike liweze kurahisisha
mawasiliano na wananchi wafanye biashara zao,”alisema Swai
Amesema wakati mwingine wanasiasa wamekua kikwazo
katika kazi za kitaalamu na kusababisha migongano isiyo ya msingi katika jamii
wakati wananchi wanahitaji miundombinu ili kuwawezesha kujiletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment