Mkuu wa mkoa Mbeya Abas Kandoro.
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya Kyela mkoani Mbeya, wamepitisha azimio la kuugawa Mkoa wa Mbeya na kupendekeza mkoa mpya uitwe Rungwe ambao makao makuu yake yatakuwa Tukuyu.
Akiwasilisha pendekezo hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kyela, Joseph Njau alisema kufuatia agizo la Rais la kuugawa mkoa ili kuwa na mikoa miwili, Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango katika kikao chake kilichofanyika Juni 7, mwaka huu ilikubaliana na suala hilo.
Alisema katika kikao hicho, kamati hiyo ilijaribu kupitia mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya wataalamu ambayo ilizingatia vigezo kadhaa kama vile jiog
rafia ya eneo lenyewe, historia ya wilaya husika, shughuli za kiuchumi zilizopo.
“Mapendekezo yaliyofikiwa katika baraza hilo, ni kuwa mkoa mpya uitwe Rungwe na makao yake makuu yawe katika mji wa Tukuyu na kuwa mkoa huo mpya utaundwa na Wilaya za Kyela, Rungwe na halmashauri ya Busokelo na Ileje sambamba na kuifanya halmashauri ya Busokelo kuwa wilaya kamili,” alisema.
Alisema Mkoa Mbeya, utabaki kuwa na Halmashauri ya Jiji, Halmashauri ya Wilaya Mbeya, Mbozi, Momba, Mbarali na Wilaya Chunya kwa sababu wilaya hizo zina uhusiano wa kijiografia tofauti na hizi za kusini.
Kwa upande wake, Diwani Kata ya Ngonga, Kileo Kabomonga alisema Mkoa wa Mbeya ndio uliokuwa umebakia kuwa na ukubwa kati ya mikoa yote nchini.
Katika kikao hicho, madiwani asilimia 99 walikubali kuwa mkoa uwe Rungwa na baadhi yao walitaka mkoa uitwe Rungwe, jambo ambalo waliliafiki. CHANZO MTANZANIA.
No comments:
Post a Comment