Mbunge wa Arumeru Mashariki akiwa hospitalini jioni hii |
Kiongozi wa Chadema aliyetambulika kwa jina la Teddy Ndossi na dereva wa Nassari. Dereva wa Nassari Guardian Palangyo amepigwa mdomoni amevunjwa meno mawili, na kwa sasa wamempiga Katibu wa Chadema wa eneo hilo anayeitwa Kilongola, wapo Kituo cha Polisi Makuyuni kutafuta msaada zaidi.
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Monduli ,Amani Sironga amesema kupitia kituo cha Radio Sunrise cha jijini Arusha kuwa wasomali hao wamekua wakimfatilia kwa muda mrefu baada ya kujulikana Nassari ndiye Wakala Mkuu wa Chadema katika Kituo hicho.
Habari za uhakika zinasema mbunge huyo hivi sasa amelazwa katika hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center maarufu kwa jina la Selian kwa matibabu zaidi .
NASSARI ALONGA
Akiongea na Blog hii Mbunge huyo amesema ameponea chupchupu kupoteza maisha baada kushushiwa kipigo kikali na kufanikiwa kuwatishia kwa silaha aliyokuwa nayo na kukimbia.
Amedai kuwa baada ya kufanikiwa kuondoka na gari lake akiwa na anafatwa na watu hao alifanikiwa kuliacha gari eneo Makuyuni mjini na kuchukua pikipiki kuelekea Minjingu akiwa anaugulia maumivu makali.
"Baada ya kufika Minjingu nilijitambulisha kwa askari wa doria waliokuwepo na baadaye kufanikiwa kurudi Arusha kwa njia ninayoijua mimi,"alisema

Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center(Selian)alikolazwa mbunge wa Arumeru Mashariki,Joshua Nassari |
No comments:
Post a Comment