Pages

May 6, 2013

Rais Kikwete awateua Msolla, Mwandu



6th May 2013
Chapa
Mbunge wa Kilolo (CCM), Profesa Peter Msolla.
Rais Jakaya Kikwete amemteua, mbunge wa Kilolo (CCM), Profesa Peter Msolla kuwa Mshauri Mkuu wa Makamu wa Rais.

Taarifa iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, jijini  Dar es Salaam, ilisema kuwa uteuzi huo ulianza Mei 2, mwaka huu.

Pia, taarifa hiyo ilisema rais Kikwete amemteua, Justine Peter Mwandu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Taarifa hiyo ilieleza kuwa uteuzi huo ulianza tangu Aprili 28, mwaka huu. Mwandu kabla ya kuteuliwa na rais kuwa mkurugenzi, alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu katika Shirika hilo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...