Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas |
Arusha
Jeshi la Polisi linawashikilia na kuwahoji
watuhumiwa 12 wanaodhaniwa kuhusika na tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea
katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti jijini
Arusha jumapili iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari leo,Kamanda wa Polisi mkoani hapa,Liberatus
Sabas amesema upelelezi wa awali umekamilika na majalada ya
watuhumiwa yamepelekwa kwa Mwanasheria wa serikali kwa hatua zaidi.
Amewataja wanaoshikiliwa na jeshi hilo kuwa ni
Victor Ambrose Calist(20),Jeseph
Yusuph Lomayani(18)waendesha Bodaboda wakazi wa Kwa Mrombo jijini Arusha, George Batholomeo
Silayo(23)mfanyabishara na mkazi wa Olasiti,Arusha,Mohamed Sulemani
Said(38)Mkazi wa Ilala,Dar es Salaam,Said Abdallah Said(28)raia wa Falme za
Kiarabu.
Sabas aliwataja wengine kuwa ni
Abdulaziz Mubarak(30)mkazi wa Abudhabi,raia wa Saudi Arabia,Jassini
Mbaraka(29)mkazi wa Bondeni jijini Arusha,Foud Saleem Ahmed(28)mkazi wa Falme
za kiarabu na Said Mohsen mkazi wa Najran,Falme za Kiarabu ambao bado
wanaendelea kuhojiwa.
Wakati huo huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ameahidi
kutoa kiasi cha Sh 50 milioni kwa atakayetoa taarifa zitakazowezesha
kukamatwa kwa waliofanya kitendo hicho cha kigaidi.
No comments:
Post a Comment