Gazeti la
chama tawala cha china, People’s Daily ambalo limezoea kuwa kitovu cha
kusambasa habari, sasa limejikuta likiwa habari baada ya watu wenye
fikra za kitukutu kuona jengo jipya la gazeti hilo limefanana na nyeti
za kiume.
Jengo hilo
lenye urefu wa mita 150, hivi sasa bado linaendelea kujengwa jijini
Beijing. Kutokana na muundo huo usiokua wa kawaida, picha za kibunifu
zikaanza kuibuka katika website ambayo ni kama “Twitter ya China,”
inayoitwa Sina Weibo.
Watu wengi
wameeleza kuwa kwa kutumia ubunifu kidogo tu wa photoshopping, unaweza
kuambatanisha picha ya jengo hilo, ambalo raia wamelipa nickname “Giant
Penis” au “Uume mkubwa,” katikati ya “miguu” ya jengo lingine maarufu
nchini humo ambalo ni makao makuu ya kituo cha TV cha China Central
Television (CCTV,) linalojulikana kwa nickname ya “Big Underpants”
building au Jengo la Chupi Kubwa.
Habari za
utani huo zilifikia wakubwa nchini humo ambao walikerwa na kuamua
kuwaharibia watu raha zao kwa kuamuru website ya Sino Weibo ku-block
search zote zinazotafuta picha au habari za jengo hilo. Kwa sasa Wachina
wakitafuta jengo hilo, wanakutana na ujumbe “kuendana na sheria, kanuni
na sera husika, matokeo ya utafutaji wako (search results) hayawezi
kuonyeshwa.
Mwandishi wa
Reuters Anita Li amesema “hii inaonyesha frustrations miongoni mwa
vijana watumiaji wa internet nchini China, na pia inaonyesha ni kiasi
gani “wakubwa” wako sensitive kwa hata vitu vidogo vya kipuuzi online.”
source-laivu
No comments:
Post a Comment