Arusha
Zaidi ya
Dola za Marekani 158 milioni zinahitajika ili kumaliza matatizo ya maji katika
jiji la Arusha kutokana na miundombinu ya zamani kuchakaa na idadi ya watu
kuongezeka.
Akizungumza
juzi,Mkurugenzi wa Mamlaka maji safi na maji taka mjini Arusha(Auwsa)Mhandisi
Ruth Koya alisema kumekuwa na malalamiko
kutoka kwa wananchi juu ya huduma wanazotoa bila kufahamu changamoto
wanazokabiliana nazo.
Alisema kwa
sasa mahitaji ya maji kwa siku ni lita za ujazo milioni 93, huku kwa siku uwezo wa Auwsa ni lita za ujazo milioni 45 na kiasi kinachopotea ni kati ya asilimia 30
hadi 36.
Mhandisi
Koya alisema kwasasa mamlaka inatumia mikakati ya muda mfupi kulingana na
kiwango cha pesa wanachopata ili
kuhakikisha wananchi wanapata huduma za maji.
Katika
mpango huo kisima cha zamani cha Moshono ambacho kilikuwa na uwezo wa kutoa
lita 16,000 kwa saa baada ya kuboreshwa kinatoa lita 36,000 kwa saa moja wakati
visima vipya vimechimbwa kwenye eneo la Sombetini chenye uwezo wa kutoa lita za
ujazo 60,000 kwa saa.
Kisima
kingine kimechimbwa eneo la Sokon I chenye uwezo wa kutoa lita 30,000 kwa saa
huku maeneo yanayotarajiwa kunufaika ni
pamoja na Sokon I,Engosheraton na Uswahilini.
No comments:
Post a Comment