Na
Mustafa Leu, Arusha.
HALMASHAURI za
wilaya mkoani Arusha, zimetakiwa kuhakikisha zinasimamia sheria ya misitu
kikamilifu ili kudhibiti ukataji miti hovyo sanjari na kuhakikisha
zinatoa hati miliki za misitu kwa vijiji ili misitu isikatwe hovyo na
kuharibu mazingira.
Kauli hiyo
imetolewa na jana na mkuu wa wilaya ya Arumeru,Nyirembe Munasa , alipokuwa
akizindua kampeni ya mkoa wa Arusha, ya upandaji miti iliyofanyika katika kata
ya Olerien eneo la Sakina ,katika halmashauri ya Arusha DC.
Akizindua
kampeni hiyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, Munasa,
amesema mkakati wa serikali mkoani humo ni kuhakikisha inapandwa miti mingi ya
asili kwa lengo la kutunza na kuimarisha Ikolojia ya uoto wa asili.
Amesema kuwa ili
miti isikatwe hovyo lazima halmashauri zihakikishe zinasimamia sheria ya misitu
ipasavyo ikiwemo miti ya asili ,ambayo uoto wake umeshaanza kutoweka kutokana
na kuharibiwa kunakosababishwa na ukataji miti hovyo katika maeneo mbalimbali
na misitu ..
Amesema mkoa huo
unakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo mwamko mdogo wa wananchi unaotokana na
utamaduni katika swala zima la kupanda miti na kuhifadhi mazingira
Mkuu huyo wa
wilaya amekiri kuwa mkoa huo mwaka jana haukufikia lengo la kupanda miti
milioni 1.5 ambapo mkoa umepanda miti milioni 1.4 tu
Amelipongeza
shirika la Youth With A Mission ( YWAM)lenye makazi yake wilayani Arumeru,
kwa kutoa miti 194,880, ambayo ni asili aina ya Jakaranda,
ambayo imepandwa katika kampeni hiyo katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
Awali Afisa
maliasili mkoa wa Arusha, Julius Achula, alisema kuwa mkoa huo mwaka huu
umepanga kupanda miti milioni 5.5 ikiwemo ya asili ambayo imewekewa mkazo
zaidi.
Amesema
kulingana na takwimuza upandaji miti mkoa huo umefanikiwa kupanda miti milioni
4,140,000 ambayo ni sawa na 79% kila mwaka yautekelezaji wa lengo la
kupanda miti milioni 5,230,000
Amesema , wilaya
nyingi mkoani humo zimeshindwa kufikia malengo ya kupanda miti milioni
1,5000,000 kutokana na changamoto mbalimbali ambazoni pamoja na
mabadiliko ya tabianchi, ambayo yanaathiri ukuaji wa miti.
Changamoto
zingine ni mifugo inayozurura hovyo, na kuharibu miti, shughuli za kilimo,
kando kando ya ya vyanzo vya maji, ufinyu wa bajeti ,ukataji wa miti
iliyopandwa ,uhaba wa vitendea kazi pamoja na mwamko mdogo walionao
baadhi ya wananchi katika swala zima la utunzaji wa miti.
Amesema mkoa kwa
kushirikiana na asasi binafsi unaendelea kuelimisha wananchi umuhimu na faida
za upandaji miti katika maeneo yao.Kauli mbiu ya mwaka huu ni “tupande miti ili
tuhifadhi mazingira kwa maendeleo endelevu “
No comments:
Post a Comment