Na Mwandishi Wetu
WAZIRI
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa jana usiku
amefanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na kubaini
mawakala wa meli wanaotoa huduma katika bandari hiyo hawafanyi kazi saa
24 kama Serikali ilivyoelekeza.
Prof.
Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA)
kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa mawakala wote waliokiuka
agizo la Serikali la kutoa huduma bandarini kwa saa 24.
"Kati
ya Mawakala wa Meli nane ambao tumewatembelea usiku huu ni wakala mmoja
tu ndiye tuliyemkuta akitoa huduma kwa saa 24 hivyo SUMATRA katika
kipindi cha siku saba hatua za kinidhamu na kisheria zichukuliwe kwa
wote wanaokiuka utaratibu huu na nipewe ripoti ya hatua
zilizochukuliwa," alisema Waziri Prof. Mbarawa.
"Katika
ukaguzi huu tumegunduwa kuwa mawakala wengi wanaacha watoa huduma
wasiostahili, wakiwemo walinzi kufanya kazi nyakati za usiku ambao
hawawezi kutoa huduma inayostahili usiku na kuendelea kutoa huduma
asubuhi jambo ambalo sio sahihi," amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa ameelezea kuridhishwa kwake na huduma zinazotolewa na taasisi
za Serikali pamoja na benki, isipokuwa kwa taasisi ya Atomiki Enegy
ambayo ameitaka ijieleze kwanini haifanyi kazi kwa saa 24 kama Serikali
ilivyoagiza.
Profesa Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Bandari (TPA), Mamlaka ya Maji Safi na Maji
Taka
jijini Dar es Salaam (DAWASCO) kuhakikisha maji safi na salama
yanapatikana bandarini hapo kwa ajili ya kuhudumia meli zinazoingia na
kutoka na mapato yanayopatikana katika huduma hiyo ya maji kujulikana.
Waziri
Mbarawa katika ziara yake ya kushtukiza aliambatana na maofisa wa
SUMATRA ili kujionea wenyewe ukiukwaji wa agizo la Serikali na
kusisitiza nia ya Serikali kuitaka Bandari ya Dar es Salaam kufanya kazi
saa 24 ni kuiwezesha kushindana na bandari nyingine katika ukanda wa
Bahari ya Hindi na kuongeza mapato.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akifanya
mahojiano na mmoja wa maofisa wa Bandari ya Dar es Salaam baada ya
kukagua kama huduma zinatolewa saa 24 kama Serikali ilivyoelekeza.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza
kwa simu na mmoja wa maofisa wa Bandari ya Dar es Salaam baada ya
kutembelea ofisini kwake.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiondoka
katika eneo linalotolewa huduma za kibenki bandarini jana usiku mara
baada ya kukagua kama huduma zinatolewa saa 24 kama Serikali
ilivyoelekeza.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati)
akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu
na Majini (SUMATRA), Giliadi Ngewe.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa pamoja na
maofisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA),
wakishuhudia moja ya wakala wa meli akiwa amefunga ofisi kinyume cha
maelekezo ya Serikali ya kufanya kazi saa 24.
No comments:
Post a Comment