Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akifungua mkutano mkuu wa mwaka
wa chama Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma uliofanyika mapema
leo mjini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akizungumza na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa
Dodoma wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofanyika
mapema leo mjini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Dodoma Bw. Edwin Kunambi akizungumza wakati wa mkutano
mkuu wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma uliofanyika mapema
leo mjini Dodoma.
Baadhi
ya wanachama wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (Press
Club) wakifuatilia mkutano huo mapema leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Chama Cha waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma Bw.Herbet Chidawali
akitoa maelezo mafupi ya namna chama hicho kinavyotekeleza majukumu yake
kwa ufanisi pamoja na changamoto zinazokikabili kwa sasa.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Khalifa Kondo akizungumza na
wanachama wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (Press Club)
wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika mapema leo mjini
Dodoma.
Na. Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Serikali
kupitia Idara ya Habari ya MAELEZO imesema itatoa kipaumbele kwa
waandishi wa habari wa Dodoma kwa kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo
kutokana na mkoa huo kuwa na matukio mengi ya Kitaifa na Kimataifa
pamoja na kutembelewa na wageni wa Kimataifa.
Hayo
yameelezwa leo mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi alipokuwa akiongea wakati wa
Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Kanda ya Kati (The
Central Press Club (CPC)).
“Nawathibitishia
kuwa Serikali sasa iko Dodoma, Dunia sasa inategemea kusikia mambo
mengi kutoka Dodoma. Shughuli za Kitaifa na Kimataifa zitakuwa
zikifanyika hapa Dodoma ,” alisema Dkt. Abbasi.
Amesema
mkoa huo utakuwa unapokea wageni mbalimbali wa Kimataifa hivyo ni
lazima waandishi wa habari wa mkoa huo wawe na uelewa wa mambo ya
Itifaki na diplomasia ili kuwasaidia katika kutekeleza majukumu yao ya
kila siku.“Lazima tubadilike hata katika uvaaji wetu,
kwani sasa tunaenda kukutana na viongozi wakubwa wa nchi na wa
Kimataifa,” aliongeza Dkt. Abbasi.
Aidha
amesema, Idara ya Habari MAELEZO itaandaa mafunzo mafupi katika maeneo
mbalimbali ya tasnia ya habari ikiwemo masuala ya itifaki na mambo ya
diplomasia ili kuwajengea uelewa waandishi hao.Hata hivyo,
Dkt. Abbas amesema Idara yake itatafuta ufadhili kwa mabalozi
mbalimbali yaliyopo hapa nchini ili waandishi hao wakajifunze namna
vyombo vya habari vya Kimataifa vinavyofanya kazi.
“Mwaka
2017 tulifanikiwa kupata ufadhili wa ubalozi wa China na waandishi Kumi
walienda China, Bado hatujajua ni waandishi wangapi watafanikiwa kwenda
mwaka huu, lakini tutao kipaumbele kwa waandishi wa habari walioko
Dodoma,” alisisitiza Dkt. Abbasi.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa CPC Habel Chidawali amesema waandishi wa
habari walioko mkoani humo walikuwa na changamoto ya kutoweza
kujiendeleza katika tasnia ya habari kutokana na vyuo vilivyopo mkoani
humo kutokuwa na kozi ya masuala ya habari.
“Kama
viongozi wa CPC tumetembelea baadhi ya vyuo vilivyopo mkoani hapa na
kuvishawishi kuanzisha kozi ya masuala ya habari katika vyuo vyao. Vyuo
vitatu vimetuahidi kuanzisha kozi hiyo mwaka huu,”alisema Chidawali.Amesema
kuwa ni mategemeo yao kuwa, waandishi wengi watajiendeleza kwa mwaka
huu jambo ambalo litawaongezea weledi katika kazi zao za kila siku hasa
kwa kipindi hiki ambapo sasa Serikali yote ipo mkoani humo.
Mkoa
wa Dodoma tayari umepokea viongozi wakuu wa nchi wawili yaani Makamu wa
Rais mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na
Mawaziri, Manaibu Waziri na Watumishi wa Serikali zaidi ya 3000. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajia
kuhamia mkoani humo muda wowote mwaka huu.
No comments:
Post a Comment