Baadhi ya mafundi na wasaidizi wao wakiendelea kujenga nyumba za Polisi jijini hapa (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha) |
Moja ya lori lililobeba mifuko ya Saruji iliyotolewa na kampuni ya Tanga Cement kwa Jeshi la Polisi mkoani Arusha . |
Na Rashid Nchimbi wa
Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi la Polisi mkoani hapa, limepokea jumla ya tani hamsini
sawa na mifuko elfu moja ya Saruji yenye thamani ya shilingi Milioni kumi na Mbili
na Laki Tano toka kampuni ya Saruji yaTanga (Tanga Cement) ili ziweze kusaidia
ujenzi wa nyumba za Askari wa Jeshi hilo ambalo hivi karibuni walipatwa na
majanga ya moto yaliyosababisha nyumba za familia 13 kuungua na kuteketeza
karibu kila kitu.
Akipokea shehena hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo
aliishukuru Kampuni ya Tanga Cement kwa kujitoa na kutambua mchango wa askari katika
kuimarisha usalama, na kuahidi kusimamia
ili ujenzi huo kasi yake iongezeke.
Alisema mbali na Kampuni hiyo pia aliwaomba watu wengine
binafsi pamoja na Makapuni mengine waige mfano toka kwa kampuni hiyo kuisaidia
jamii hasa katika sekta mbalimbali kama vile elimu, afya na majanga kama haya.
Kamanda Mkumbo pia alitumia fursa hiyo kushukuru watu binafsi
, makampuni, taasisi pamoja na majeshi
ya Ulinzi na Usalama kama vile Jeshi la Wananchi (JWTZ), Jeshi la Polisi
Kilimanjaro, Chuo cha Polisi Moshi na Jeshi la Magereza.
Wengine ni kiwanda cha Magodoro cha Tanfoam, kiwanda cha A to
Z, Ofisi ya Mwanasheria mkoani hapa, Green Valley School na Kampuni ya Otterlo
Business Corporation Ltd (OBC) pamoja na watu binafsi ambao walitoa msaada wa
fedha, Chakula, Saruji nguo pamoja na Magodoro.
Kwa upande wake Meneja Biashara wa kampuni hiyo Bw. Peet Brits
alisema kwamba, wao kama kampuni wameweka mkazo kusaidia katika elimu, afya,
maendeleo ya Jamii pamoja na mazingira lakini kwenye majanga mbalimbali kama
vile ajali za moto.
Alisema kwamba anafahamu kazi zinazofanywa na Jeshi la Polisi
katika kudumisha usalama ambapo unasaidia kuvutia mazingira mazuri ya
kibiashara hapa nchini. Alisema wametoa msaada huo ili usaidie kujenga makazi
ya familia za askari.
Bw. Brits alisema anajua walichochangia hakiwezi
kutosheleza lakini wanaamini kitasaidia
kwenye ujenzi wa nyumba hizo na kuzitaka kampuni pamoja na taasisi kusaidia Jeshi la Polisi ambalo linaimarisha usalama
hali ambayo inasaidia kuweka mazingira mazuri ya kibiashara.
Familia 13 za Jeshi hilo mkoani hapa zilikosa makazi siku ya
tarehe 27/09/2017 baada ya nyumba zao zilizopo katika moja ya Kambi za Polisi
kuungua kwa moto uliotokana na hitilafu ya umeme ulitokea muda wa saa 12:45
Jioni.
Post a Comment