Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Jumamosi Septemba 30,2017
ameweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya
msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School”
iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika manispaa
ya Shinyanga.
Mbali
ya kuweka jiwe la msingi pia ameendesha harambee kwa ajili ya kupata
shilingi milioni 200 kwa ajili kukamilisha ujenzi huo,ambapo wazazi na
walezi wameshiriki katika harambee hiyo.
Akizungumza
katika shule hiyo,Matiro aliwapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi kwa
kujitoa kwa hali na mali kusaidia shule hiyo ambayo imejizolea sifa
lukuki kwa utoaji wa elimu bora.
“Shule
hii imejizolea sifa nzuri,hii ni miongoni mwa shule bora kabisa
nchini,kila mzazi anapenda mtoto wake asome kwenye shule nzuri,ukifika
Shinyanga ukauliza shule gani nzuri,utatajiwa shule hii,nimeambiwa siri
ya mafanikio haya inatokana na maono na utayari wa wazazi na marafiki
kuisaidia shule hii”,alifafanua Matiro.
“Sisi
kama serikali tunaunga mkono sekta binafsi,kutokana na shule hii kufanya
vizuri,ni ukweli usiopingika kuwa imeleta ushindani mkubwa kwa shule
zetu za serikali,nasi kwa upande wa shule zetu za serikali hatuna budi
kuiga, tuje kujifunza nini wanafanya hapa Little Treasures”,aliongeza
Matiro.
Aliwaasa
wazazi na walezi mkoani Shinyanga kupeleka watoto shule kwani urithi
pekee kwa watoto ni elimu na wala siyo mali ambazo hupotea kirahisi
sana.
Katika
hatua nyingine alizitaka shule za taasisi binafsi kutoza ada
zinazoendana na hali ya uchumi wa wazazi huku akiwasihi wazazi kutoa
ushirikiano katika shule akitolea mfano wa shule ya Little Treasures
ambayo imekuwa karibu zaidi na wazazi na walezi wa wanafunzi. Mkurugenzi
wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic alisema ili kukamilika
kwa jengo la bwalo la chakula jumla ya shilingi milioni 200
zinahitajika na tayari uongozi wa shule umetenga shilingi milioni 50
hivyo bado zinahitajika shilingi milioni 150.
Naye
Meneja wa shule hiyo,Wilfred Mwita alisema pindi jengo hilo
litakapokamilika litatumika kama sehemu ya wanafunzi na wafanyakazi wa
shule hiyo kula chakula lakini pia kwa ajili ya shughuli mbalimbali
ikiwemo michezo na mikutano.
Akisoma
risala,Mkuu wa shule hiyo,Paul Kiondo alisema shule hiyo yenye mchepuo
wa Kiingereza ina wanafunzi wa bweni na kutwa ilianza na wanafunzi wanne
pekee na sasa ina jumla ya wanafunzi 662 kati yao,wavulana ni 304 na
wasichana 318 na imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani mbalimbali.
Jumla
ya shilingi milioni 15 zimepatikana katika harambee hiyo ya kuchangia
ujenzi wa bwalo la chakula,ambapo wazazi na walezi pamoja na marafiki wa
shule hiyo wamechangia huku Mkuu wa wilaya Shinyanga Josephine akitoa
shilingi Milioni 2 pamoja na mifuko 30 ya saruji.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (wa pili kulia) akiwasili
katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery &
Primary School”.-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiweka jiwe la msingi katika
jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures
“Little Treasures Nursery & Primary School”.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisoma maandishi baada ya
kuweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya
msingi Little Treasures.
Maandishi
yakisomeka kwa lugha ya Kiingereza yakiwa na maana ya 'Jiwe la Msingi
limewekwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro leo Septemba
30,2017'.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipanda mti wa kumbukumbu
baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika
shule ya msingi Little Treasures.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimwagilia maji mti alioupanda katika shule ya Little Treasures.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiondoka katika eneo
panapojengwa jengo la Bwalo la chakula katika shule ya msingi Little
Treasures.Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo,Tilulindwa Sulusi. ![](https://3.bp.blogspot.com/-JOsLxR59XxQ/Wc_O22fwrpI/AAAAAAAASO4/liNv2OjRv3sI8kBGiDattkB5lBmpQ3VPwCLcBGAs/s640/UF3A5481.JPG)
Wanafunzi
wa shule ya msingi Little Treasures wakimwongoza Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro katika maaandamano kuelekea eneo la mkutano
kwa ajili ya harambee kuchangia ujenzi wa bwalo la chakula katika shule
hiyo.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika maandamano hayo.Wa
kwanza kushoto mbele ni Mkurugenzi wa shule ya msingi Little
Treasures,Lucy Dominic,kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya shule
hiyo,Tilulindwa Sulusi.
Meza
kuu: Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Kulia ni
Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic,kushoto ni
Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo,Tilulindwa Sulusi.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika shule ya
msingi Little Treasures ambapo aliipongeza shule kuwa na mazingira
mazuri ya kujifunzia wanafunzi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliwasisitiza wazazi kupeleka watoto shule kwani ndiyo urithi unaofaa kwa watoto.
Meneja
wa shule ya Little Treasures, Wilfred Mwita akizungumza wakati wa
harambee hiyo ambapo aliwaomba wazazi na walezi wa wanafunzi pamoja na
marafiki kuendelea kushirikiana na shule hiyo.
Mkurugenzi
wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic akizungumza wakati wa
harambee hiyo ambapo aliishukuru serikali kwa kuendelea kushirikiana
shule hiyo ili kuboresha kiwango cha elimu mkoani Shinyanga na nchi kwa
ujumla.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Little Treasures,Tilulindwa Sulusi akitoa neno.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures, Paul Kiondo akisoma risala.
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakicheza ngoma ya Kijaluo mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Wanafunzi wakicheza muziki.
Wazazi na walezi waliohudhuria mkutano huo wa harambee kuchangia ujenzi wa bwalo la chakula.
Meneja
wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga,Said Pamui naye alikuwepo katika
harambee hiyo ambapo alichangia shilingi 500,000/- kusaidia ujenzi wa
bwalo la chakula katika shule hiyo.
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakicheza ngoma ya Kikurya.
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiimba ngonjera.
Wazazi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.
MC Mama Sabuni akifanya yake.
Wazazi wakiwa katika eneo la tukio.
Walimu wa shule ya msingi Little Treasures wakifuatilia yaliyokuwa yanajiri.
Wazazi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Waandishi wa habari wa magazeti ya Daily News na Habarileo,Suleiman Shagata na Kareny Masasy wakiwa katika eneo la tukio.
Waandishi wa habari John Mponeja wa Channel Ten na Getruda Mallya wa Radio Faraja wakifurahia jambo.
Meneja
wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga,Said Pamui (kushoto) akiwa na
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya msingi Little Treasures, Tilulindwa Sulusi
wakiondoka katika shule hiyo baada mkutano wa harambee.
Picha ya kumbukumbu mbele ya jengo la utawala shule ya msingi Little Treasures.-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment