SERIKALI
inatekeleza Programu ya miaka mitano ya Maendeleo ya Sekta ya Maji
nchini (2016/21) ambapo pamoja na mambo mengine imekusudia kuboresha
hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Miji Mikoa ya Mikoa kutoka
asilimia 86 hadi 95.
Taarifa
ya Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji inaonesha kuwa Idadi
ya wateja waliounganishiwa huduma hiyo imeongezeka kutoka 405,095 mwezi
Machi 2016, hadi wateja 432,772 mwezi Machi, 2017 ambapo asilimia 97 ya
wateja hao wamefungiwa dira za maji ili kulipia huduma ya maji kulingana
na matumizi.
Pamoja
na ongezeko hilo la uzalishaji wa maji bado mahitaji ya maji ni makubwa
katika maeneo ya Miji Mikuu ya Mikoa ikiwemo Jiji la Dar es Salaam,
hatua iliyoilazimu Serikali kuwekeza katika miundombinu ya maji na
kuzijengea uwezo mamlaka za maji ili kuongeza upatikanaji wa huduma ya
majisafi na salama katika Jiji hilo.
idadi
ya maunganisho kwenye mtandao wa majisafi ya Jiji la Dar es Salaam
imeongezeka kutoka wateja 155,000 mwezi Machi, 2016 hadi kufikia wateja
182,721 mwezi Machi, 2017, kutokana na kuongezeka kwa makusanyo ya
maduhuli ya mauzo ya maji kutoka Tsh. Bilioni 7.1 Machi, 2016 hadi Tsh.
Bilioni 8.3 Machi, 2017.
Akizungumza
na Waandishi wa habari hivi karibuni Jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA),
Mhandisi Romanus Mwang’ingo anasema mamlaka hiyo inatekeleza miradi
mbalimbali inayolenga kuongeza upatikanaji maji, kusambaza maji maji
katika Jiji La Dar es Salaam na baadhi ya Miji ya Mkoa wa Pwani.
Mwang’ingo
anasema mahitaji ya maji katika eneo la huduma la DAWASA ikijumuisha
miji ya Kibaha na Bagamoyo ni mita za ujazo 544,000, ambapo uzalishaji
wa rasilimali hiyo kutoka vyanzo vya visima na mitambo ya Ruvu Juu, Ruvu
Chini na Mtoni ni mita za ujazo 502,000 kwa siku.
Anaongeza
hadi sasa Mamlaka hiyo tayari imekamilisha miradi mbalimbali
inayokusudia kuongeza hali ya upatikanaji maji Jijini Dar es Salaam
ikiwemo upanuzi wa mtambo wa maji wa Ruvu Chini uliowezesha kuongeza
kiwango cha uzalishaji wa maji kutoka lita za ujazo 180,000 hadi
270,000.
“Katika
mtambo wa maji wa Ruvu Chini pia tumefanikisha ulazaji wa bomba kuu la
mita 1.8 kutoka Ruvu chini hadi matenki ya chuo kikuu cha Ardhi,
vilevilw kuanza ujenzi wa ofisi za kuendeshea mradi huu” anasema.
Kuhusu
Mtambo wa Ruvu Juu, anasema DAWASA imekamilisha ujenzi wa njia mpya ya
umeme mkubwa kutoka Chalinze hadi Mlandizi pamoja na kuongeza kiwango
cha uzalishaji wa maji kutoka lita 82,000 hadi lita 196,000.
Kwa
mujibu wa Mwang’ingo anasema ili kuhakikisha kuwa kiwango cha maji
kilichoongezeka kinawafikia wananchi, DAWASA inatekeleza mradi wa
uboreshaji wa mfumo wa usambazaji maji katika maeneo ya Jiji la Dar es
Salaam na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani.
Akifafanua
zaidi anasema kazi zilizofanyika katika mradi huo ni pamoja na ujenzi
wa matenki 9 ya kuhifadhi na kusambaza maji yenye ukubwa wa kuhifadhi
maji lita milioni 3 hadi 6, ujenzi wa vituo nne vya kusukuma maji pamoja
na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji yatakayokuwa na urefu wa
kilometa 477.
“Maeneo
yatakayonufaika na mradi huu ni pamoja na Salasala, Bunju, Wazo,
Makongo, Changanyikeni, Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kiromo, Kitoprni, Ukuni,
Kerege, Buma, Mataya na ukanda maalum wa EPZA” anasema.
Mhandisi
Mwang’ingo anasema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuimarisha
mitandao ya maji kuwa katika mfumo rasmi na hivyo kufanya maji
kugawanywa kwa ufanisi na uwiano mzuri zaidi hususani katika maeneo ya
milimani ambapo maji hayakuweza kuwafikia wananchi wengi.
Kwa
mujibu wa Mwang’ingo anasema katika kudhibiti upotevu wa maji, DAWASA
itafunga mita maalum katika maeneo ya kupokea maji na matoleo yake hatua
inayolenga kujua kiasi kamili cha maji kilichoingia katika eneo husika
na kiasi kilichogawanywa kwa wananchi.
“Tofauti
na mita za kawaida, mita hizi zitakuwa zinapeleka taarifa moja kwa moja
katika ofisi za DAWASCO ambapo vifaa maalum vitafungwa na itakuwa
rahisi kutambua ni wapi maji yanapotea na hivyo kutafuta njia ya
kuyadhibiti”
Kuhusu
Miradi ya ukusanyaji na uondoaji wa majitaka anasema DAWASA imeanza
mradi wa ujenzi wa mitambo mitatu mikubwa ya kusafisha majitaka
itayojengwa katika maeneo ya Jangwani, Mbezi Beach na Kurasini hatua
inayolenga kuongeza kiwango cha kusafisha majitaka kufikia asilimia 30
ifikapo mwaka 2020.
Mhandisi
Mwang’ingo anasema Gharama za jumla za miradi hiyo ni Dola za Marekani
Milioni 600, ambapo miradi hiyo itatekelezwa kwa awamu na awamu ya
kwanza inatarajia kuanza ndani ya mwaka huu wa fedha 2017/18.
Anasema
mitambo hiyo mipya itawezesha kuzalisha gesi asilia na umeme
utakaotumia kuendeshea mitambo, hatua itayosaidia kupunguza gharama za
umeme na pia maji yatakayokuwa yametibiwa yatauzwa na kutumika katika
shughuli mbalimali ikiwemo kupozea mitambo na umwagiliaji.
Akizungumzia
kuhusu mradi wa uchimbaji visima katika Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo, Mwang’ingo anasema DAWASA imebuni mradi huo ili kukabiliana na
changamoto ya upungufu wa maji katika baadhi ya maeneo ya Halmashauri
Mpya ya Ubungo katika kipindi ambacho Manispaa hiyo ikisubiri
utekelezaji wa miradi mikubwa ya usambazaji maji.
“Mradi
utahusu uchimbaji wa visima 10 katika maeneo ya Kwa Mvungi, Gogoni,
Mpiji Kibesa, Makabe-Mbezi Luis, Tegeta A, Matosa, Kingazi B, Malamba 2,
Kingazi A, na Luguruni, ambapo uchimbaji visima umekamilika na
mkandarasi anasafisha na kupima wingi na ubora wa maji” anasema.
Akiwasilisha
Hotuba ya makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2017/18,
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge anasema hali ya
upatikanaji wa huduma ya maji katika Miji Mikuu ya Mikoa na miji midogo
imeendelea kuimarika na kuweza kupunguza kero ya uhaba wa maji safi kwa
wananchi wa miji hiyo.
Waziri
Lwenge anasema Serikali inaendelea kukamilisha ujenzi wa miradi ya
uzalishaji wa maji na miundombinu ya kusambaza maji ili kuboresha hali
ya upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam
na Miji ya Kibaha na Bagamoyo.
Anasema
katika jitihada za kuimarisha vyanzo vya maji, Wizara yake imeendelea
kuhamasisha wananchi kuhusu utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji
pamoja na utafutaji wa vyanzo vingine vya maji ikiwemo ujenzi wa mabwawa
ya kimkakati na uchimbaji wa visima virefu.
Serikali
inatekeleza miradi mikubwa ya maji ili kuhakikisha kuwa Tanzania
inafikia malengo ya kitaifa na kimataifa katika upatikanaji wa huduma ya
maji safi na salama.
Ni
wajibu wa wananchi kulinda miundombinu ya maji ikiwemo kudhibiti
upotevu wa maji katika mifumo ya usambazaji wa maji kunakosababishwa na
kuvuja kwa mabomba ya maji.
No comments:
Post a Comment