Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Seriel
Mchembe mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) kwa ziara
ya kikazi ya siku moja. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt.
Stephen Kebwe. (Picha na OWM).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Gairo, Bw.
Ahmed Shabiby mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) kwa
ziara ya kikazi ya siku moja. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe nawa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo,
Bi. Seriel Mchembe (Picha na OWM).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro,
Bw. Cliford Tandari mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017)
kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Mvomero. (Picha na OWM).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akipanda mti nje ya Ofisi ys Mkuu wa Wilaya ya
Gairo mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) ikiwa ni
sehemu ya kuadhimisha Siku ya Upandaji Miti Kitaifa. Wengine ni viongozi
wa Mkoa na Wilaya wakishuhudia. (Picha na OWM).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimwagilia mche alioupanda nje ya Ofisi ys Mkuu
wa Wilaya ya Gairo mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017)
ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Upandaji Miti Kitaifa. Wengine ni
viongozi wa Mkoa na Wilaya wakishuhudia. (Picha na OWM).
Viongozi
na watumishi wa Wilaya ya Gairo wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa (hayupo pichani) katika mkutano aliouitisha mjini Gairo Juni 3,
2017. (Picha na OWM).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi na watumishi wa Wilaya ya
Gairo (hawapo pichani) katika mkutano aliouitisha mjini Gairo Juni 3,
2017 (Picha na OWM).
………………………………………………………………………………………..
* Ni la sh. milioni 213/- la fedha za maendeleo.
*Ataka apewe taarifa ifikapo Juni 30.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw.
Clifford Tandari aitishe kikao na uongozi wa Halmashauri ya Kilosa na
kupata kauli yao ni lini watalipa zaidi ya sh. milioni 210 wanazodaiwa
na Halmashauri ya Gairo.
“Katibu
Tawala itisha kikao cha Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkuu wa Wilaya na
Mkurugenzi wa Halmashauri, waseme ni lini watazileta fedha hizo ambazo
zilitumwa kwao wakati Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ikiwa haijafungua
akaunti zake,” amesema.
Ametoa
agizo hilo leo (Jumamosi, Juni 3, 2017) wakati akizungumza na viongozi
wa mkoa wa Morogoro, wilaya ya Gairo na watumishi wa Halmashauri ya
Gairo mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa na wilaya katika kikao
kilichofanyika Gairo mjini
“Kilosa
ni lazima wazilipe hizo fedha. Katibu Tawala simamia zoezi hilo na kama
watachelewa, uzikate moja kwa moja kwenye fedha yao wanayoletwa kutoka
Ofisi ya Rais (TAMISEMI). Nataka nipewe taarifa ya maamuzi hayo kabla
Juni haijaisha,” amesema.
Mapema
akitoa taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Siriel
Mchembe alisema wanaidai Halmashauri ya Kilosa sh. 233,228,679 ambazo
ziliingizwa huko wakati wilaya hiyo inaanzishwa na hawakuwa wamefungua
akaunti ya wilaya.
“Fedha
hizi zilikuwa zinapitia Kilosa wakati wilaya ya Gairo imeanzishwa kwa
kuwa kipindi hicho wilaya ya Gairo ilikuwa bado haijafungua akaunti.
Fedha hizi zinajumuisha ruzuku ya uendeshaji, mapato ya ndani na miradi
ya maendeleo,” alisema.
Alisema
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) iliagiza wilaya
ya Kilosa ilipe deni hilo kabla ya Juni 2016 lakini hadi sasa
wameshalipa sh. milioni 20 tu ambapo sh. milioni 10 zililipwa Desemba
2015 na nyingine milioni 10 zililipwa Mei 2017.
Akisisitiza
kuhusu makusanyo ya mapato, Waziri Mkuu amewakumbusha watumishi hao
kuwa Serikali imekwishatoa agizo la kutumia mashine za kielektroniki
kukusanya mapato ifikapo Julai mosi.
“Makusanyo
ya mapato ya ndani ni eneo muhimu sana. Tumeshaagiza, mwisho wa kutumia
mifumo ya kawaida ni Juni 30. Kuanzia Julai mosi, kila eneo ni lazima
litumie mashine za kielektroniki,” alisema Waziri Mkuu.
Alihoji
ni kwa nini Halmashauri ya Gairo ililenga kukusanya sh.milioni 889.5
lakini kufikia Aprili mwaka huu, makusanyo halisi yalikuwa ni sh.
milioni 356.2 sawa na asilimia 40.
Alitumia
fursa hiyo kuwapongeza Mamlaka ya Mapato (TRA) ya wilaya hiyo ambao
hadi kufikia Aprili, 2017 wameweza kukusanya sh. milioni 601.5
ikilinganishwa na makadirio yao ya kukusanya sh. milioni 471 kwa mwaka.
Waziri Mkuu aliwapongeza kwa sababu wamevuka lengo kwa asilimia 127.6.
Waziri
Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku ya wilaya hiyo, asubuhi alipanda
mti kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ikiwa maadhimisho ya siku ya upandaji
miti hapa nchini.
Pia
alikagua mradi wa maji wa kijiji cha Chakwale, na mradi wa visima 10
ambayo imekuwa na mgogoro kwa muda mrefu. Pia atazungumza na wananchi wa
Gairo mjini kwenye mkutano wa hadhara.
No comments:
Post a Comment