Katibu
Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara
kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akivishwa skafu na
mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji
wa Kahama alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule
hiyo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara
kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akisaini kitabu cha wageni
alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari
Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara
kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akioneshwa baadhi ya jumbe
zilizopo katika mabango zilizoandaliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya
Save the Children, alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita
katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa
Kahama.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara
kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akiongozwa na Mkuu wa Shule
ya Sekondari Mwendakulima Bi.Neema Daniel iliyopo Halmashauri ya Mji wa
Kahama kupanda mti wa kumbukumbu, alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato
cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya
Mji wa Kahama.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara
kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akikata utepe kuashiria
kuanza kwa mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari
Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii)
Bi.Deodatha Makani akiongea jambo na Mkurugenzi wa Ubora na Maendeleo
wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Save the Children Amy Schmiot mahafali
ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo
Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Katibu
Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama Bw.Timothy Ndaya akiongea na
wanafunzi na wazazi waliohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita
katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa
Kahama ambapo alieleza dhamira ya ofisi yake kuendelea kusimamia ubora
wa shule hiyo pamoja na kushughulikia changamoto zake.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara
kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akiongea na wanafunzi na
wazazi waliohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya
Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama ambapo
aliwataka wazazi kuwalinda watoto na ndoa za utotoni pamoja na
kuwasisitiza kuendeleza vipaji vyao.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara
kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akitoa vyeti pamoja na
zawadi kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo
Halmashauri ya Mji wa Kahama alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha
sita ya shule hiyo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara
kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja
na wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari Mwendakulima
iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama pamoja na walimu wao.
Baadhi
ya wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari Mwendakulima
iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama wakifuatilia mahafali.
……………………………………………………………………
Na Hassan Silayo-MAELEZO
Wazazi
nchini wametakiwa kutekeleza wajibu wao kwa watoto kwa kuhakikisha
wanawaendeleza na kuwawezesha wafanikishe ndoto zao kwa kuwaepusha na
ndoa pamoja na mimba za utotoni.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga katika
Mahafali ya 5 ya kidato cha sita ya shule ya sekondari Mwendakulima
iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Bi.Sihaba
amesema kuwa wazazi wanajukumu la kuhakikisha wanawalea na kuwalinda
kwani wazazi wanahaki ya kisheria ya kuwalinda watoto dhidi ya viashiria
vyote vinavyoweza kuwaweka katika mazingira hatarishi.
Bi.Sihaba
aliongeza kuwa wazazi na walezi wana haja ya kushirkiana na serikali
katika kuwalinda watoto wakike kwani watoto wa kike ni nyenzo muhimu
hasa kwenye mpango wa serikali katika kuelekea uchumi wa kati kupitia
viwanda.
Aidha,Bi.Sihaba
kuwa Serikali imefanya marekebisho ya Sheria ya Elimu sura namba 33
inayotoa katazo kumpa ujauzito motto wa shule chini ya miaka 18 hivyo
wazazi wahakikishe wanalisimamia kwa pamoja ili kuweza kufanikisha
sheria.
Naye
Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama Bw.Timothy Ndaya
alieleza dhamira ya ofisi yake kuendelea kusimamia ubora wa shule hiyo
pamoja na kushughulikia changamoto zake ili kuendana na mipango ya
serikali ya awamu ya tano katika kuipa kipaumbele sekta ya elimu.
Mkurugenzi
wa Ubora na Maendeleo wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Save the
Children Amy Schmiot amesema kuwa mahafali hayo ni ishara ya ushirikiano
mzuri wa wazazi,walezi pamoja na uongozi wa shule utakaowezesha watoto
hao kuvuna kile walichokipanda kwenye miaka 6 ya masomo yao.
Mkuu
wa shule hiyo Bi.Neema Daniel alimuahidi Bi.Sihaba kuendelea kufanya
vizuri katika mitihani ya kitaifa pamoja na kuiomba serikali kuwashika
mkono hasa katika kurekebisha miundombinu ya shule hiyo ikiwamo mabweni
na uzio wa shule.
Naye
Mhitimu katika mahafali hayo Rose Bryton amewataka wazazi na walezi
kutekeleza maagizo ya serikali ya kuwalinda watoto ili kuwawezesha
kutimiza ndoto na matarajio yao kielimu.
Akitoa
ushauri kwa wazazi wenzake Bi Rebecca Peter amewataka wazazi kuachana
na mila zilizopitwa na wakati za kuwaozesha watoto wa kike katika umri
usiotakiwa kisheria bali kuwaendeleza kufikia ndoto zao.
Jumla
ya wanafunzi 143 wamehitimu masomo ya kidato cha sita katika shule ya
sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama
No comments:
Post a Comment