Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi amegawa hati
miliki za ardhi 122 kwa wananchi wa Lamadi Mkoa wa Simiyu wakati
alipofanya ziara yake mikoa ya kanda ya ziwa kuhamasisha ulipaji kodi ya
pango la ardhi na suala la urasimishaji wa makazi holela.
Wananchi
hao 122 ni wale waliofanikiwa kulipia michango yote, hivyo kuondokana
na makazi holela na kuishi katika makazi rasmi. Hata hivyo jumla ya
wananchi 5,200 wa Lamadi Mkoa wa Simiyu washapimiwa maeneo yao kwa ajili
ya urasimishaji, na watapatiwa hati zao mara tu baada ya kukamilisha
michango stahili.
Katika
ziara hiyo, waziri Lukuvi amefika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza na
kufanya ukaguzi wa mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi wilayani hapo
na kugundua kati ya wakazi 35,000 wanaotakiwa kulipa kodi ya ardhi
28,000 wameishapelekewa hati ya madai.
Waziri
Lukuvi pia ametembelea Idara ya Ardhi ya wilayani Nyamagana na kukagua
mafaili ya kumbukumbu za wananchi kuhusu taarifa za ardhi ikiwemo
masuala ya hati na kukugundua baadhi ya viongozi hawajalipa kodi ya
pango la ardhi. Mmoja ya viongozi hao ni Mbunge wa Kwimba Shannif
Mansoor ambaye hajalipa kodi ya pango la ardhi tangu 2010 kiasi cha
shilingi milioni 529.
Aidha
katika wilaya hiyo ameongea na wananchi wa Nundu kata ya Meko, mbali ya
kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi papo hapo, amewahimiza
kuchamkia fursa ya kurasimisha makazi yao na kupata hati ili kuzipa
thamani ardhi zao na kujitanulia fursa za uchumi.
Magere
Mugeta mkazi wa Lamadi mkoani Simiyu akipokea hati ya kumuliki ardhi
kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa
William Lukuvi.
Janet
Magige mkazi wa Lamadi mkoani Simiyu akipokea hati ya kumuliki ardhi
kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa
William Lukuvi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi
akiwasisitiza wakazi Lamadi mkoani Simiyu umuhimu wa kumiliki ardhi kwa
hati kwa kuwaonesha moja ya hati zinazotolewa kwa wananchi.
Wakazi
wa Lamadi mkoani Simiyu wakishangilia pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi kwa kuwawezesha kupata
Hati za kumiliki Ardhi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi
akikagua moja ya faili katika masijala ya Ardhi ya Ilemela Mkoani Mwanza
akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela (mwenye kofia).
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi
akikagua mfumo wa kodi wa manispaa ya Nyamagana mkoani Mwanza ili
kubaini wadaiwa wa kodi ya Ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akiongea na wakazi wa Ilemela mkoani Mwanza.
Baadhi
ya wakazi wa Ilemela mkoani Mwanza wakimsikiliza kwa makini Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi alipokuja
kusikiliza kero zao za ardhi.
No comments:
Post a Comment