Na Karama Kenyunko- blogu ya jamii.
Mkulima
mmoja Samwel Nicodem Bwandu 38, amehukumiwa kwenda jela miaka 20 baada
kupatikana na hatia ya kukutwa na vipande nane vya meno ya tembo vyenye
thamani ya milioni 60.
Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Akisoma
Hukumu, huyo hakimu shahidi amesema kuwa, upande wa mashtaka umeweza
kuthibitisha mashtaka bila ya kuacha shaka kuwa kweli Bwandu alikutwa na
meno ya tembo lakini haukuweza kuthibitisha kuwa alikuwa akijihusisha
na biashara hiyo.
Hata
hivyo, mahakama hiyo,imemuachia huru Kidamisi Kidarageda Kidiwami, Mkazi
wa Iringa baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka
dhidi yake kuwa alihusika katika tuhuma hizo za meno ya tembo.
Watuhumiwa
wote wawili, Bwandu na Kidawami walikuwa wakituhumiwa kwa makosa ya
kupatikana na nyara za serikali ambazo ni vipande nane vya meno ya tembo
vyenye thamank ya milioni 600 na Kijihusisha na nyara hizo zenye
thamani ya milioni 900.
Hakimu
Shahidi amesema, amezingatia ushahidi wote uliotolewa na upande wa
mashtaka na utetezi wa washtakiwa na kuridhika kwamba mshtakiwa Kidawami
hakuhusika katika kutenda makosa hayo.
"Hakuna
shahidi yeyote aliyefika mahakamani hapo na kuthibitisha kuwa mshtakiwa
wa Kidawami alihusika na tuhuma hizo, isipokuwa shahidi namba tano
ambaye nae alikuwa na ushahidi wa kusikia tu", amesema hakimu Shahidi"
Ameongeza
kuwa, kwa upande wa mshtakiwa Bwandu upande wa mshtakiwa wa upande
umeweza kuthibitisha bila shaka kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo kwani
hata aliposachiwa alikuwa na nyara hizo.
Kabla
ya kumsomea adhabu yake baada ya kipatikana na hatia, hakimu Shahidi
aliuliza upande wa mashtaka kama alikuwa na kitu chochote cha kusema
ambapo, Wakili wa serikali, Elia Athanas aliiomba mahakama itoe adhabu
stahiki kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa jamii nzima kwani
vitendo vilivyofanywa na mshtakiwa vinachafua taswira ya nchi kimataifa
Ameongeza
adhabu hiyo siyo tu itakuwa fundisho bali itasaidi dunia nzima ijue
Tanzania iko serious katika kutatua tatizo lanuharibifu wa maliasili na
kuirudisha nchi katika hadi yake.Naye mshtakiwa Bwandu katika utetezi wake aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwani ameishakaa sana gerezani.
"
Mahakama inakuhukumu kwenda jela miaka 20 na hapo nimezingatia na muda
uliokaa gerezani lakini kwenye suala la faini lipo kisheria ambapo MTU
anatakiwa kulipa mara kumi ya gharama za nyara alizokutwa nazo lakini
katika suala hilo mahakama inakaa kimya kwa kuwa haiwezi kutoa adhabu
isiyotekelezeka.
Aidha
ameongeza kuwa iwapo upande wa mashtaka ukidhibitisha kuwa mshtakiwa
anamali ambazo zinaweza kutaifishwa walete maombi mahakamani.
Alisema
Maliasili ni zawadi kutoka kwa Mungu ambayo ndio Eden tuliyonayo
watanzania ambayo tunapaswa kuiheshimu n kuifurahia wote siyo mtu mmoja
mmoja, haiwezekani kuachiwa MTU afanye anachotaka kwani maliasili hizi
hutuletea fedha za kigeni.
Ilidaiwa
kuwa Juni 28, 2015 huko Mabibo external, washtakiwa walikutwa na
vipande nane vya meno ya tembo vyenye thamani y milioni 600 ambavyo ni
sawa na tembo wawili.
No comments:
Post a Comment