Katika
kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani,Klabu ya
waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club- SPC)
Mei 3,2017 imefanya mkutano na wadau wa habari mkoani Shinyanga kujadili
namna klabu hiyo ilivyo na wajibu wa kuendeleza amani katika jamii.
Mgeni
rasmi katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel mjini
Shinyanga alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack
aliyekuwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na
usalama mkoa wa Shinyanga.
Siku
ya Uhuru wa Vyombo vya Habari huadhimishwa duniani kote kila ifikapo
tarehe 3 mwezi Mei ya kila mwaka ambapo pamoja na maadhimisho ya kitaifa
kufanyika kitaifa jijini Mwanza,lakini yamefanyika pia katika kila mkoa
nchini yakiwa na kauli mbiu inayosemayo “Klabu za Waandishi wa Habari
zina wajibu wa kuendeleza amani katika jamii”.
Awali
akitoa hotuba yake,Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa
Shinyanga,Kadama Malunde alisema Klabu za waandishi wa habari zina
wajibu wa kuendeleza amani katika jamii hivyo kuwataka waandishi wa
habari kutumia kalamu zao vizuri kuandika habari zinazojenga utaifa na
kuleta mshikamano katika jamii.
Malunde
alisema Klabu za waandishi zinawaweka pamoja waandishi wa habari hivyo
kupitia umoja huo zinawabijika kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza
amani katika jamii kwani pasipo na amani hakuna maendeleo.
Aliongeza
kuwa kutokana na nguvu ya vyombo vya habari,amani katika jamii
itaendelea kuwepo endapo tu waandishi wa habari watazingatia maadili ya
kazi yao na kuepuka kushabikia mambo yasiyo na maana.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack
aliwataka waandishi wa habari kutanguliza utanzania na uzalendo katika
habari wanazoandika.
“Ndugu
zangu waandishi wa habari mnajukumu kubwa la kulinda amani ya nchi
hii,tumieni kalamu zenu vizuri,epukeni kuandika habari za kujenga hofu
na mnapoandika basi msiegemee upande mmoja,sikilizeni hata upande wa
pili ili kutenda haki”,alieleza mkuu wa mkoa.
Katika
hatua nyingine Telack aliwahamasisha waandishi wa habari kuimarisha
mshikamano walionao na kujiendeleza kielimu huku akiwashauri kuanzisha
miradi itayowakomboa kiuchumi kwani fursa mbalimbali za kiuchumi zipo
mkoani humo.
“Nitoe
wito kwa waandishi wa habari kuunga mkono sera ya uchumi wa
viwanda,andikeni habari kuhusu viwanda na kilimo na kupitia umoja wenu
anzisheni mashamba ya pamba na alizeti na mnao uwezo wa kuanzisha
viwanda vidogo ili kuinua uchumi wenu,andikeni proposal mnaweza
kuanzisha hata kiwanda cha maziwa”,aliongeza Telack.
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack. Kushoto ni Kamanda wa
jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro.Kulia ni
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Bw. Kadama
Malunde
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack akifungua mkutano wa
wadau wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya
habari duniani ngazi ya mkoa wa Shinyanga
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack. Kushoto ni Kamanda wa
jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro.Kulia ni
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama
Malunde
Katikati
ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde
akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack
Wa
kwanza kulia ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga Anna Maria Yondani
akifuatiwa na Kanali Mussa Kingai ambaye ni mwakilishi wa vikosi JWTZ
Shinyanga kwenye kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti
wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akizungumza
wakati wa mkutano wa wadau wa habari mkoa wa Shinyanga kuadhimisha siku
ya uhuru wa vyombo vya habari duniani Mei 3,2017
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akitoa hotuba ukumbini
Wadau wa habari wakiwa ukumbini
Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Stephen Wang'anyi akisisitiza jambo ukumbini
Wadau wakiwa ukumbini
Mwandishi wa habari Suleiman Shagata akichangia hoja ukumbini
Mwenyekiti
wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde(kushoto) na
katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Stephen
Wang'anyi wakiwa ukumbini
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akiongoza majadiliano ukumbini
Kaimu Mwenyeti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Shaaban Alley akizungumza ukumbini
Mratibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Nunu Abdul akiandika dondoo muhimu
Wadau wakiwa ukumbini
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Wadau wakiwa ukumbini
Mkutano unaendelea
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza ukumbini
Msaidizi wa Askofu Kanisa kuu la KKKT Shinyanga Usharika wa Ebenezer Trafaina Assery Nkya akizungumza ukumbini
Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategire akizungumza ukumbini
Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga Anna Maria Yondani akizungumza ukumbini
Kanali
Mussa Kingai ambaye ni mwakilishi wa vikosi JWTZ Shinyanga kwenye
kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga akichangia hoja ukumbini
Mdau Gelard Ng'ong'a kutoka shirika la Rafiki SDO
Afisa habari kutoka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mji wa Kahama (KUWASA) bwana Mkama akichangia hoja
Mdau wa habari bwana Chief Abdallah Sube akichangia hoja
Bwana John Myola kutoka Shirika la AGAPE Shinyanga akizungumza ukumbini
Mkurugenzi Msaidizi Radio Faraja,bwana Anikazi Kumbemba akizungumza ukumbini
Mwakilishi wa Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga,Bi Alice Mazoko akichangia hoja
Mwandishi wa habari Patrick Mabula akifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack akizungumza ukumbini
Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack,wadau wa habari na waandishi wa habari
Picha
ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack,wajumbe wa
kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga na waandishi wa habari.
Picha zote kwa hisani ya Shinyanga Press Club
Picha zote kwa hisani ya Shinyanga Press Club
No comments:
Post a Comment