Mkuu
wa Mkoa wa Simiiyu, Anthony Mtaka akifungua kikao cha usuluhishi baina
ya mwekezaji wa Mwiba Holdings na wadau wa maendeleo mkoani Simiyu
kilichofanyika mwishoni mwa wiki.
MKUU
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amefanikiwa kumaliza mgogoro wa muda
mrefu kati ya mwekezaji katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA)
Makao iliyopo wilayani Meatu, na baadhi ya vijiji vinavyounda jumuiya
hiyo.
Mwekezaji
huyo Mwiba Holdings, amekuwa na mgogoro wa mipaka, mkataba wa kumiliki
ardhi na uanzishaji wa ranchi na baadhi ya vijiji hivyo kiasi cha
kusababisha kuwa na mahusiano mabaya na wananchi ambao wamekuwa
wakisusia misaada mbalimbali inayotolewa na mwekezaji huyo.
Hata
hivyo, chanzo halisi cha mgogoro huo kimegundulika kuwa ni viongozi wa
baadhi ya vijiji ambao wamekuwa wakipigania maslahi yao binafsi huku
wakisambaza taarifa za upotoshaji juu ya mwekezaji huyo na kujenga chuki
kwa wananchi.
Vijiji
vinavyounda WMA ya Makao ni pamoja na Makao, Iramba ndogo, Sapa,
Mwangudo, Jinamo, Lukale, Mbushi, Mwabagimu na Sunga. Baadhi ya viongozi
hao wa vijiji pia wamekuwa wakisambaza taarifa potofu kwa wananchi
kwamba Mkuu huyo wa mkoa na mkuu wa wilaya ya Meatu wamehongwa na
mwekezaji ili kuwakandamiza wananchi, jambo lililothibitika kuwa si la
kweli.
Kutokana
na mgogoro huo kuzidi kuota mizizi huku uongozi wa CCM Mkoa wa Simiyu
nao ukichukua upande, Mtaka alilazimika kuitisha kikao cha usuluhishi
kilichoshirikisha wadau wote wakiwamo Kamati ya Siasa ya CCM mkoa na
wilaya, viongozi na watendaji wa serikali ngazi ya mkoa na wilaya,
viongozi wa vijiji tisa vinavyounda WMA Makao, mwekezaji na wadau
wengine akiwamo Mbunge wa Meatu na Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Akizungumza
katika kikao hicho kilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini hapa, Mtaka
aliwakemea viongozi wanaoeneza taarifa potofu wilayani humo na
kusababisha shughuli za maendeleo kukwama huku akiahidi kuwachukulia
hatua zinazostahili viongozi wa namna hiyo. “Katika masuala ya maendeleo
ya wananchi sina mzaha. Nipo tayari kuwa kiongozi unpopular
(asiyependwa) ili mradi shughuli za maendeleo za wananchi zinaenda
mbele.
“Mgogoro
na Mwiba umekuwa kama mkuki mnaojichoma wenyewe kila siku kwa sababu
wenyewe ndiyo mlioingia mikataba na mwekezaji wakati sisi hatukuwapo na
wala hatuna maslahi yoyote binafsi hivyo acheni maneno maneno, kaeni
chini mzungumze tusonge mbele,” alisisitiza Mkuu huyo wa mkoa.
“Mmefikisha malalamiko, tena kwa maandishi hadi kwa Waziri Mkuu lakini
uhalisia ni kuwa mengi mliyopeleka hayana ukweli, ni hisia na mengine ni
fitna tu. Sasa wekeni kila kitu hadharani hapa, tumalize suala hili leo
na tujikite zaidi katika mambo ya maendeleo,” alisema.Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Simiyu, Dk Titus Kamani akizungumza katika kikao cha
usuluhishi baina ya wananchi wa Meatu na Mwekezaji wa Mwiba Holdings
kilichofanyika mjini Mwanhuzi mwishoni mwa wiaki.Mkuu
wa Mkoa wa Simiiyu, Anthony Mtaka akifungua kikao cha usuluhishi baina
ya mwekezaji wa Mwiba Holdings na wadau wa maendeleo mkoani Simiyu
kilichofanyika mwishoni mwa wiki
Kuhusu
mgogoro wa mpaka hasa katika kijiji cha Buhongoja ambako alama ya mpaka
yenye namba 314 inadaiwa kusogezwa kinyemela kwa umbali wa kilomita 10,
Mkuu huyo wa mkoa alizitaka pande zinazohusika kukutana na kutatua
tatizo hilo kwa kurejea katika eneo la awali bila ya mikwaruzano yoyote.
Aliamuru pia pande zinazohusika katika suala la mkataba wa umiliki wa
ardhi,kukaa meza moja na kuacha mambo ya kukimbilia kwa wasuluhishi
ambao wamekuwa wakidai fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kwa
maendeleo ya vijiji au wilaya ya Meatu.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini aliahidi kupeleka wataalam
watatu watakaosaidiana kutatua mgogoro huo wa umiliki wa ardhi
watakaosaidiana na wake wa wilaya ili kutatua suala hilo ndani ya wiki
mbili. Awali, Mwenyekiti wa Kijiji cha Makao, Anthony Phillipo alieleza
kuwa kijiji kilazimika kupelaka suala hilo kwenye Tume ya Usuluhishi wa
Migogoro Dar es Salaam ambako kijiji walishindwa kulipa gharama za
usuluhishi huo walizotozwa na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Simiyu, Dk. Titus Kamani alieleza chama hicho tawala
kusikitishwa na mgogoro huo unaokwamisha shughuli za maendeleo ya
wananchi na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho. “Ndugu
zangu, sisi tunajiandaa kushinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa
mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kwa hiyo tunawaomba
tusikubali kuingizwa katika migogoro kama hii ambayo haina tija kwa
wananchi.
“Tunataka
wakati wa uchaguzi utakapofika tushinde pila pressure (msukumo) yoyote
na tunachotaka ni mshikamano,maelewano mazuri baina ya wadau wote ili
tufanye shughuli za maendeleo kwa faida ya mkoa wetu wa Simiyu na wilaya
ya Meatu,” alisisitiza.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mpina Luhaga ambaye
pia ni mbunge wa Kisesa wilayani Meatu alisema katikA kikao hicho kuwa
mwekezaji huyo amekuwa akifuata sheria zote za nchi katika utekelezaji
wa majukumu yake na ni wazi kwamba wananchi watashindwa katika madai
yote wanayofungua katika Tume ya Usuluhishi wa migogoro.
“Mimi
nimefuatilia malalamiko haya ya wananchi serikalini na hasa Wizara ya
Maliasili na Utalii na hawa jamaa wamefuata taratibu zote na wanalipa
tozo zote wanazostahili kulipa hivyo tunapaswa kuwa waangalifu,”
alisema. Mkurugenzi wa Mwiba Holdings, Abdulkadir Mohamed Luta alisema
kuwa Kampuni hiyo ipo tayari kukaa meza moja na kusaidia usuluhishi wa
mgogoro wowote ili wajikite zaidi katika shughuli za maendeleo ya
wananchi.
Aliongeza
kwamba kampuni hiyo ilikuwa tayari kugharamia hata suala la mkataba wa
umiliki wa ardhi lililofikishwa Tume ya Usuluhishi wa Migogoro ili mradi
tu suala hilo liishe na waendelee na mambo ya maendeleo Alisema
watazifanyia kazi hoja zote zilizotolewa na wananchi katika kikao hicho
na kwamba sera ya kampuni hiyo ni kushirikiana na wananchi na wamekuwa
wakitekeleza sera hiyo kwa vitendo.
Mbunge
wa Meatu, Salum Khamis maarufu kwa jina la Mbuzi, alisema kuwa hana
mgogoro na mwekezaji yoyote lakini hatakaa kimya kutetea maslahi ya
wananchi wake ambao ndio waajiri wake kila atakapoona kuna sababu ya
kufanya hivyo.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Pius Machungwa aliahidi
kuipatia kiwanja cha kujenga ofisi Kampuni ya Mwiba Holdings katika
makao Makuu ya wilaya hiyo ili iwe karibu na wananchi, na kwamba
watashirikiana na kampuni hiyo katika shughuli za maendeleo wilayani
humo.
No comments:
Post a Comment