Makamu
wa Rais wa Klabu ya Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu jana amefungua
Tawi la kwanza la Simba mjini Bukoba na kuweza kuwaunganisha Wana Simba
wa hapa Kagera. Pia katika Uzinduzi huo wa Tawi ambalo lipo Kashabo pia
walikuwepo Wachezaji wa Simba wakiongozwa na nahodha Jonas Gerald
Mkude, Kichuya na Wengine. Piacha na Faustine Ruta, Bukoba
Pia
wameweza kumshukuru ndugu Omary Makoye, Mratibu wa Tawi wa Klabu ya
Simba kwa kuwatembelea wakiwa katika Mchakato wa kuunda Tawi hilo. Na
pia wameshukuru kwa msaada aliowapa na ulikuwa ukihitajika kwa muda huo.
Shukrani pia kwa Ndugu Sued Mkwambi kwa kukubali kuwa mlezi wao wa
Tawi.
Makamu
wa Rais wa Klabu ya Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburuakiteta na
Wanatawi na wanakagera waliokuwa eneo la Tawi hilo la Kichwabuta.
Mh.
Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu(wa pili)
kutoka kushoto akiwa na Viongozi wa Tawi la Kichwabuta lililozinduliwa
leo hii mjini Bukoba. Tawi hilo limepewa Jina la Kichwabuta kutokana na
kuenzi kazi ya Mwananchama maarufu wa Klabu ya Simba MZEE HUSSEIN OMARY
KICHWABUTA ambaye alishiriki kikamilifu kama mpenzi na Mwanachama wa
Simba katika maendeleo ya Klabu hiyo ya Simba. Tawi hilo mpaka sasa lina
Wanachama 160 waliojiandikisha na taratibu zinaendelea kuhakikisha
wanapata kadi za uanachama kulingana na utaratibu wa Klabu. Tawi
linaongozwa na Mwenyekiti Ndugu Priscus Isdory Massawe, Katibu ndg.
Fauzu BinaMungu, Mhasibu Ndg. Dickson Ishengoma, Msemaji Ndg. Miraji
Kichwabuta na Viongozi wengine ili kuhakikisha wanapata Wanachama wengi
zaidi.
No comments:
Post a Comment