Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia Watendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na Mbunge wa
Jimbo la Ilemela Mhe. Angelina Mabula (kulia) wakati wa mkutano wa
Makamu wa Rais na Watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini
Mwanza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akihutubia mbele ya Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa
mkutano wa watendaji na Halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Picha ya pamoja
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
ameunga mkono jitihada za kupambana na dawa za kulevya nchini kama hatua
ya kuliokoa na taifa janga hilo ambalo limesababisha madhara makubwa
katika jamii.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na
watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Makamu
wa Rais amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya yatakuwa ni
endelevu lengo likiwa kukomesha kabisa uuzaji,usambazaji na utumiaji wa
dawa hizo kama hatua ya kuokoa kizazi cha sasa na kijacho nchini.
Amesema
kamwe serikali ya wamu ya Tano hatarudi nyuma katika vita dhidi ya dawa
za kulenya na ameomba wananchi waendelee kutoa taarifa za siri kwa
vyombo vya dola zitakazosaidia kuwabaini watu wanajihusisha na biashara
hiyo ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kuhusu
tatizo la uvuvi haramu, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan
amewaagiza viongozi wa mikoa ya kanda ya Ziwa wakiwemo viongozi wa
Mwanza na mikoa mingine nchini kuanzisha mara moja oparesheni kali ya
kupambana na wavuvi haramu katika Ziwa Victoria ambao wamechangia kwa
kiasi kikubwa kupungua kwa samaki katika Ziwa hilo.
“Viwanda
vya samaki kwa sasa havipati samaki wa kutosha hali ambayo imezorotesha
shughuli za kuchakata samaki hivyo nawaagiza viongozi wote kupambana
ipasavyo na wavuvi haramu na kamwe wasionewe huruma” amesisitiza Makamu
wa Rais.
Makamu
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya dawa
za kulevya nchini ni muhimu yakaenda pamoja na oparesheni ya kukomesha
uvuvi haramu katika Ziwa Victoria na maeneo mengine nchini.
Amesema
wavuvi haramu wamechangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa samaki katika
maziwa mbalimbali nchini kwa sababu wanatumia nyavu haramu ambazo
zinaharibu mazalia ya samaki hivyo ni lazima hatua stahiki zichukuliwe
dhidi yao ili kukomesha kabisa tatizo hilo.
Wakati
huo huo halmashauri ya wilaya ya Ilemela, imetekeleza maagizo 14
yaliyotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa mwaka jana alipofanya ziara ya kikazi
wilayani humo likiwemo suala la watumishi wa halmashauri kukaa karibu na
maeneo ya ofisi ambapo mpaka sasa wakuu wa idara 23 wanaishi ndani ya
wilaya ya Ilemela ikilinganishwa
na hapo awali ambapo watumishi hao walikuwa wanakaa nje ya wilaya hiyo
hali ambayo inatajwa ilichangia kuzorotesha utendaji kazi kwenye
halmashauri hiyo.
Kufutia
hali hiyo, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mlezi
wa halmashauri hiyo amepongeza viongozi wa wilaya hiyo pamoja na
watendaji wa halmashauri kwa kutekeleza maagiza yake kwa haraka na kwa
wakati.
Amesema
yeye kama mlezi wa halmashauri hiyo atahakikisha halmashauri inafanya
kazi kwa ubora wa hali ya juu katika utoaji wa huduma za uhakika kwa
wananchi na kuondoa haraka changamoto mbalimbali zizowakabili wananchi
hao ikiwemo uimarishaji wa miundombinu ya barabara
No comments:
Post a Comment