Pages

August 6, 2016

Serikali Zanzibar yatilia mkazo soka la wanawake


Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar pamoja imewahasa wazazi nchini wametakiwa kutoa uhuru kwa watoto wao wa kike kucheza mpira wa miguu ili kuifikisha nchi katika ushindi na kuitangaza Kimataifa.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Hassan Mitawi alipokuwa akifungua mashindano ya Airtel Rising Stars yaliyofanyika uwanja wa Amaan.

Alisema bila ya michezo Zanzibar haiwezi kujulikana hivyo ni vyema kwa wazazi na walezi kuwapa motisha watoto wao wa kike kushiriki katika michezo hasa mpira wa miguu.

Alisema mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo wenye kutoa ajira kama ilivyo kwa wanaume lakini tabia ya baadhi ya wazazi kuwakataza watoto wao wa kike kujiingiza katika soka kuwakosesha fursa zinazotokana na mpira ikiwemo afya bora, ajira pamoja na kuchangia katika kukuza soka la wanawake nchini.

Mitawi alisema watu wanazaliwa na vipaji na vipaji hivyo vinapaswa kuendelezwa hasa kwa upande wa Zanzibar wanawake washirikiane kudumisha michezo.

Aidha aliishukuru Airtel kuzidi kukuza na kusaidia michezo nchini na kuwataka kuendelea kuwekeza katika michezo hususani soka la wanawake.

Awali Mwenyekiti wa soka la wanawake Hatima Mwalimu alisema mashindano hayo yatasaidia kuinua vipaji vitakavyoisaidia Zanzibar kushiriki katika mashindano mbalimbali.

Nae Meneja Mauzo wa Airtel Zanzibar Muhidin Mikadadi alisema “Tunajisikia fahari kusaidia mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 hapa nchini na tumejipanga kuibua vipaji vya vijana kupitia program hii. Tunafurahi kuona vijana wengi wanajitokeza kushiriki mashindano hayo na tunawashukuru ZFA na Wizara ya Michezo kuwaunga mkono katika kusaidia na kukuza michezo nchini”.

Huu ni msimu wa sita kwa mashindano ya Airtel Rising Star nchini kwa mwaka humu Zanzibar impeta nafasi ya kushiriki, jumla ya timu sita zinashiriki katika mashindano haya ni pamoja na Mwenge kutoka Wilaya ya Kusini, Kidimni Kutoka Wilaya ya Kati,New Generation Kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi, Jumbi Women kutoka Wilaya ya Kati na Bungi Sisters kutoka Wilaya ya Kati.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamanduni na Michezo Zanzibar Hassan Mitawi akikangua timu wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar Ijumaa 5 Agosti 2016.

Mchezaji wa Bungi Sister FC Agatha Peter (nyekundu) akichuana na beki wa Jumbi Woman Fighter Arafa Mbaraka wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.

Mchezaji wa Bungi Sister FC Swahiba Khamis (nyekundi) akichuana na Shamira Shaban wa Jumbi Woman wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.
Mchezaji wa Bungi FC Suzan Francis (nyekundu) akichuana na Agnes Andrew wa Jumbi Woman Fighter wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.
Mchezaji wa Bungi FC Suzan Francis (nyekundu) akichuana na Agnes Andrew wa Jumbi Woman Fighter wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.


Jumbi Woman fighter FC defender Agnes Adrew (white) runs past Bungi FC player striker Suzan Fransi (red) during the launch of Airtel Rising Stars 2016 Zanzibar. Bungi Sister won 3-0.
Mchezaji wa Bungi FC Suzan Francis (nyekundu) akichuana na Agnes Andrew wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.
Mchezaji wa Bungi Agatha Peter akichuana na Swahiba Hamis wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.
Mchezaji wa Bungi Juba Skampunda akichuana na Semeni Hamad wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar. Bungi FC ilishinda 3-0.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...