Aliyekuwa
mke wa rais wa zamani nchini Kenya Lucy Kibaki amefariki. Lucy
alifariki katika hospitali ya Bupa Cromwell mjini London. Alisafrishwa
hadi mjini Landon wiki moja iliopita kwa matibabu.Akithibitisha kifo
chake rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa kenya imesikitishwa na
kifo cha mama Lucy mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki.Katika
taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari Uhuru amesema bi Lucy amekuwa
mgonjwa kwa kipindi cha mwezi mmoja .Amesema kuwa Kenya imempoteza
mwanamke aliyechangia mengi katika maendeleo ya taifa la Kenya hususan
katika vita dhidi ya ugonjwa wa ukimwi.Rais ametuma risala za rambi
rambi kwa mtangulizi wake Mwai Kibaki pamoja na familia yake.
News Alert: Obituary: Lucy Kibaki afariki dunia
rweyemamuinfo.blogspot.com
0

Post a Comment