Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akisalimiana na Maofisa wa
Polisi katika Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya jana wakati alipokuwa
katika ziara ya kikazi katika mkoa huo wa Kipolisi.Kushoto ni Kamanda wa
Polis Kanda Maalumu Tarime na Rorya, Lazaro Mambosasa.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa Hosteli ya Polisi Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya jana
wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo wa Kipolisi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizindua Hosteli ya Polisi
katika mkoa wa Kipolis Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya jana wakati
alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo wa Kipolisi
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na wadau wa
Polisi (hawapo pichani) wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi mkoa wa
Kipolisi Tarime na Rorya ambapo alitumia kikao hicho kuwaasa kufanya
uchaguzi kwa amani na utulivu.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Tarime.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu amewataka Viongozi wa Vyama
vya Siasa katika Wilaya za Tarime na Rorya kufanya Kampeni za Kistaarabu
ili kufanikisha Uchaguzi Mkuu pamoja na kuimarisha Amani na Usalama
Wilayani humo.
IGP
Mangu aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Wadau wa Polisi
wakiwemo Viongozi mbalimbali, Vyama vya Siasa pamoja na Wagombea wa Viti
vya Ubunge na Udiwani, wakati alipokuwa katika Ziara ya Kikazi katika
Kanda Maaalum ya Polisi Tarime na Rorya.
Alisema
ili uchaguzi wa mwaka huu uweze kufanyika kwa amani, Viongozi wa Vyama
vya Siasa na Wagombea hawana budi kuwashawishi wafuasi wao kufuata
Maadili ya Uchaguzi ikiwemo kutotoleana lugha za Matusi.
IGP
Mangu alisema baada ya Uchaguzi maisha yataendelea kama kawaida hilo ni
jukumu la Wananchi wote wa Tarime kuondoa Uhasama wao katika mambo ya
Siasa kwa kuwa Siasa siyo Uhasama.
Aidha,
aliwashauri Wagombea Ubunge na Udiwani katika Majimbo ya Tarime Mjini,
Vijijini, na Rorya kukutana mara kwa mara ili kujenga kuaminiana na
kutatua changamoto zinazojitokeza katika kipindi hiki cha kampeni na
hatimaye siku ya uchaguzi Mkuu.
Kwa
upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Tarime na Rorya,
kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Lazaro Mambosasa, aliwahakikishia Wadau
wote kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vyema kukabiliana na vitendo
vyote vya vurugu vitakavyojitokeza, pamoja na kuhakikisha kila Mwananchi
aliyejiandikisha anapata fursa ya kupiga kura bila vitisho vya aina
yoyote.
Naye
Mgombea Ubunge katika Jimbo la Rorya kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi,
Lameck Airo alisema katika jimbo analogombea hakuna vurugu kwa kuwa
wamekuwa wakiheshimiana katika Kampeni ili kuepusha vurugu kwa Wagombea
na Wafuasi wao.
Kikao
hicho kilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Viongozi wa
Dini,Vyama vya Siasa, Wafanyabiashara, Asasi zisizo za Kiserikali, Wazee
wa Kimila pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya
Tarime.
No comments:
Post a Comment