Msanii wa Bongo Fleva,Khadija Shabani’Keisha’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali maeneo ya Maktaba,Posta jijini Dar.
Akizungumza na mtandao huu,Keisha alisema kuwa alikuwa akitoka
chuoni CBE na kwamba alikuwa akimfuata mumewe alipofika maeneo hayo
ndipo lilipotokea gari na kumuovateki na kuligonga gari lake.
Aidha alisema kuwa alisikia maumivu na alipokwenda hospitali kufanyiwa vipimo vilionyesha hakupata majeraha kwa ndani.
"Nashukuru Mungu nilipimwa hospitali vipimo vilionyesha sikupata
madhara yoyote kwa ndani kwani nilikuwa na wasiwasi labda niliumia kwa
ndani," alisema Keisha
No comments:
Post a Comment