Pages

September 28, 2013

HIKI NDICHO KILICHOTOKEA KATIKA KUAGA MWILI WA MKUU WA WAANDISHI WA MWANANCHI COMMUNICATION LTD MOROGORO VENACE GEORGE MHANGILWA (40) ALIYEFARIKI DUNIA SEPTEMBA 26 MWAKA HUU HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MOROGORO WAKATI WA IBADA YA KUAGA NYUMBANI KWAKE TUBUYU KATA YA TUNGI MKOANI HAPA.


Mke wa mkuu wa waandishi wa habari kampuni ya Mwananchi Communication LTD mkoa wa Morogoro, Venance George (40) Sauda Mgombelwa akilia mara baada ya kuag
a mwili wa mume wake wakati wa misa kabla ya kuanza safari ya kwenda kijiji cha Bukoti Geita kwa mazishi, Venance alifariki dunia Septemba 26 mwaka huu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ambako alilazwa. PICHA ZOTE NA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
 
 Venance George enzi za uhai wake. 
 Mwandishi wa kampuni ya IPPMEDIA mkoa wa Morogoro Devotha Minja akiwa mwenye huzuni huku akiwa amemkumbatia Hamida Shariff wa gazeti la Mwananchi Morogoro jana wakati wa kuaga mwili wa bosi wake.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera kushoto akimpa pole baba wa Venance George, Mzee George Mhakingilwa wakati wa misa ya kuaga mwili wa marehemu Venance, Kulia ni Mke wa Marehemu Sauda Mgombelwa.
Bendera akifafanua jambo huku George Mhangilwa (katikati) na Boninvetura Mtalimbo kulia wakisikiza jambo muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kusafirisha mwili wa marehemu Venance George kwenda kijiji cha Bukoti Geita kwa ajili ya mazishi. 
 Jeneza lenye mwili wa mwaandishi Venance George likiingizwa katika basi ndogo aina ya coaster tayari kw kuanza safari.
 
 Mtoto wa kiume wa Venance George, Erasto akiwa amekaa katika gari hilo.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akisali na kutoa heshima za mwisho kwa Mwananchi Venance George wakati wa zoezi la kuaga.
 Mratibu wa Morogoro Press Club Morogoro, Thadei Hafigwa akiweka shada la maua katika jeneza lenye mwili wa marehemu Venance George na kutoa heshima za mwisho.
Mratibu wa mazishi ya Venance George, Bonveture Mtalimbo akizungumza jambo.
 
 Waandi wa magazeti ya HabariLeo John Nditi kulia na Peter Kimath JamboLeo wakitoa heshima za mwishi.
 Mwandishi wa gazeti la Uhuru na Mzalendo mkoa wa Morogoro Latifa Ganzel kulia na Ester Mwimbula wa Mwananci nao wakitoa heshima za mwisho. Dastan Shekidele kulia naye akitoa heshima za mwisho katika tukio la kuaga mwili wa marehemu.
Katekesta wa kanisa la romani katoliki jimbo la Morogoro Ernest Mathey akinyunyuzia maji ya baraka katika jeneze lenye mwili wa Venance George nyumbani kwake mtaa wa Tubuyu kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro.
 Kutoka kushoto, Devotha Minja (ITV) Hamida Shariff (Mwananchi) Mwenyekiti wa Morogoro Press Club, Idda Mushi, Latifa Ganzel (Uhuru na Mzalendo) na Lilian Lucas (Mwananchi) wakifuatilia jambo wakati wa misa ya ibada ya marehemu Venance George (40) iliyofanyika nyumbani kwake mtaa wa Tubuyu kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro jana.
 Mtoto wa kwanza wa Veanace George, Ivon Veanace George akiwa mwenye huzuni wakati wa ibada hiyo.
 kutoka kushoto mstari wa nyuma, Lilian Justice (Majira) Amina Saidi (Star Tv) na Merina Robert (Mtanzania na Clouds Fm) kila mmoja akiwa ameweka pozi la majonzi wakati wa tukio hilo.
 Mwandishi wa Tanzania Daima, Joseph Malembeka kulia akisaidiana na mwenzake kumpa msaada mwanamke ambaye aliishiwa nguvu wakati wa tukio la kuaga.
 Mwenyekiti wa Morogoro Press Club Idda Mushi akitoa neno juu ya msiba huo.
 Mwenyekiti wa CCM wilaya Morogoro Fikiri Juma akizungumza jambo
 Katibu wa mbunge wa jimbo la Morogoro kupitia CCM, Abdullaziz Abood, Mourice Massala naye akizungumza jambo

Huyu ndiye Andrew Mpasa ambaye ni Meneja Mauzo gazeti la Mwananchi Morogoro akihakikisha kila jambo lina kwenda sawa katika msiba huo.
 Timu ya watumishi wa Mwananchi Communication LTD katika msiba huo.

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU VENANCE GEORGE.
Marehemu Venance George Mhangilwa alizaliwa mnamo 8/12/1973 Bukoti wilaya ya Geita.

ELIMU:
-Marehemu alisoma katika shule ya msingi Bugogo kuanzia mwaka 1981 mpaka mwaka 1987 alipohitimu elimu yake ya msingi. 
-Mnamo mwaka 1988 alianza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Forest Hill iliyopo Morogoro na kuhitimu kidato cha sita mnamo mwaka 1994.
-Mwaka 1995 alijiunga katika chuo cha uandishi wa habari na kuhitimu mwaka 1996.

AJIRA:
Marehemu alianza kazi ya uandishi wa habari katika kampuni ya,
 -Uhuru Publication Limited, 1996-1998.
-Kuna Entarprises Company Limited, 1998-1999.
-Village Travel And Transport Project (VTTP), 2001-2003.
-Swiss-Contact Tanzania Limited, 2001-2003
-Mwananchi Communication Limited, 2003 mpaka mauti yalipomkuta.
Pia alijiendeleza kimasomo katika chuo kikuu huria cha Tanzania ambapo alitakiwa kuhitimu shahada yake ya mawasiliano ya umma mwezi wa 12 mwaka huu 2013.

MWISHO:
-Marehemu alikuwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu na kifua hali iliyopelekea kwenda kulazwa katika hospitali ya Aga Khan iliyopo jijini Dar es salaam na kupata nafuu, Baada ya kurudi nyumbani hali ilbadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa katika hospitali ya Holly Cross Mission iliyopo mkoani Morogoro na baadaYe kuhamishiwa katika hospitali kuu ya mkoa wa Morogoro. 
Marehemu alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani , baada ya siku kadhaa hali ilibadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro hadi umauti ulipomkuta mnamo tarehe 26/09/2013 saa 9:15.
-Marehemu ameacha mjane na watoto wawili wa kike na wa kiume.

SHUKRANI:
-Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote waliokuwa pamoja na sisi tangu marehemu alipoanza kuugua mpaka leo hii , shukrani ziwafikie wafanyakazi wenzake, ndugu, jamaa na marafiki wa karibu. Maelezo haya kwa mujibu wa Mratibu wa mazishi, Bonveture Mtalimbo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...