Pages

May 8, 2018

KAMPUNI YA ULINZI YA SGA YAFURAHIA USHINDI WA KWANZA MAADHIMISHO YA MEI MOSI

Meneja wa kampuni ya ulinzi ya SGA,Daudi Mungi aliyeshika kikombe akifurahi na wafanyakazi wenzake katika hafla ya kuwapongeza wafanyazi bora iliyofanyika ofisini kwao Esso jijini Arusha,walitangazwa washindi wa kwanza katika kundi la watoa huduma wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi mkoa wa Arusha.

Wafanyakazi wa kampuni binafsi ya ulinzi ya SGA wakifurahia kikombe cha mshindi wa kwanza kwa taasisi zinazotoa huduma ofisini kwao eneo la Esso jijini Arusha .   

Na Mwandishi Wetu,Arusha
Kampuni binafsi ya ulinzi ya SGA imewapongeza kwa kuwapa vyeti wafanyakazi wake 20 walioshiriki matembezi ya Siku ya Wafanyakazi duniani yaliyofanyika kimkoa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Katika hafla ya kuwapongeza iliyofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo eneo  Esso jijini hapa,Meneja wa kampuni hiyo,Daudi Mungi alisema ni tukio la aina yake kwa kampuni hiyo tangu ianze kazi zake hapa nchini kupata kombe.

"Tumekua wenye furaha sana kuzawadiwa kombe la mshindi wa kwanza katika kundi letu,hili tukio linatupa chachu ya kuongeza bidii kwenye utendaji wa kazi zetu na kuhakikisha wateja wetu wanakua salama,"alisema Mongi

Katibu wa chama cha wafanyakazi wa Chodawu mkoa wa Arusha,Jeremia Meliari alisema ushindani katika kundi hilo ulikua mkali na kuwapongeza kwa ushindi walioupata.

Aliwataka waongeze tija kwa kutoa huduma bora kwa wateja wao na kuifanya kampuni hiyo kukua zaidi na kutoa fursa za ajira kwa vijana wengi ili wasijiingize kwenye vitendo vya uhalifu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...