Wanachama
wa PST wakifuatilia ufunguzi wa Kongamano
|
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akitoa hotuba katika ufunguzi wa
kongamano la 49 la Chama cha Wafamasia
Tanzania
|
Wajumbe
wa kongamano wakiendelea kufuatilia Hotuba ya Ufunguzi
|
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(Kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Chakula na dawa Hiti Silo katika Kongamano la wafamasia
linalofanyika katika Jiji la Arusha.
|
Na Nteghenjwa
Hosseah, ARUSHA
SERIKALI imesema
kuwa inaanza kufanya maboresho kwa kuandaa na kuhakikisha Sera ya
Uboreshaji wa Viwanda vya Dawa vilivyopo nchini kwa kuwawezesha na
kuwajengea uwezo wenye viwanda nchini ili waweze kuzalisha dawa na kupunguza
uagizaji wa dawa kutoka nje ya nchi.
Kauli hiyo
ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo kwa
niaba ya Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista
Mhagama alipokuwa akizungumza katika Kongamano la 49 la Chama Cha
Wafamasia Tanzania (PST),linalofanyika jijini hapa kwa siku mbili.
Akizungumza kwa
niaba ya Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,alisema kuwa kutokana na
umuhimu wa sekta hiyo ya dawa, Serikali inaangalia taaluma hiyo kwa macho
mawili kwa lengo la kuiboresha ili iweze kutoa huduma bora.
"Wizara yangu
inaangalia taaluma hii kwa macho mawili katika kuhakikisha kuwa sekta ya dawa
inaboreka na inakua na hatimaye kuweza kukuza uchumi wetu, kwa kuwawezesha na
kuwajengea uwezo wenye viwanda nchini ili waweze kuzalisha zaidi ikiwa ni pamoja
na kuwahakikishia soko ndani ya nchi na kupunguza uagizaji wa dawa kutoka nje
ya nchi na hivyo kuwa na dawa bora, salama na zenye ufanisi"
"Endapo
tutazalisha dawa zetu wenyewe hii itatupunguzia gharama zisizo za lazima
kuagiza dawa nje ya nchi, sambamba na hili pia tunaboresha vyuo vya Wafamasia
ili waweze kutoka wataalamu bora wa masuala haya ya madawa,”alisema Gambo
Akizungumzia suala
la wizi wa dawa katika hospitali za serikali,alisema kuwa Serikali haina mchezo
na yoyote atakayokiuka maadili ya taaluma hiyo na kuwa watawachukulia hatua
kali za kisheria ili wananchi wapate huduma bora za dawa.
"Mbali na
changamoto ya upungufu wa dawa, wafanyakazi wasio waadilifu ambao wanatumia
nafasi zao vibaya wanashirikiana na baadhi ya wafanyabiashara na kuuza
dawa, hili ni suala muhimu PST jadilianeni suala la maadili kwani hatua za
kisheria dhidi yao zitachukuliwa"alisema
Awali Rais wa PST,
Michael Kishiwa, aliiomba Serikali kuongeza udahili wa wanafunzi wa famasia
wakiwemo mafamasia wasaidizi ili kutoa dawa sahihi kwa wagonjwa.
Alisema hivi sasa
idadi ya watanzania ni kubwa, lakini wataalamu wa dawa Wafamasia ni 1,200, hali
inayochangia kuwepo kwa watoa huduma hiyo wasio na sifa.
Alisema kutokana
na kukosekana wanataaluma kumekuwepo na changamoto kubwa ya baadhi yao kukiuka
maadili na wengine kufanya kazi ya utoaji dawa pasipokuwa na uelewa nayo, hali
ambayo hatari kwa afya za binadamu.
Kishiwa alisema
kazi kubwa ya chama chao kuhakikisha inasimamia ubora wa utoaji huduma ya dawa
na kusimamia maadili, ili wananchi wapate dawa sahihi na kuzitumia ipasavyo.
“Tunashirikiana na
baraza la usajili la wafamasia katika kukemea vitendo hivyo vya ukiukwaji wa
maadili na ndiyo maana tunaiomba serikali iongeze udahili na vyuo vinavyotoa
taaluma hii"alisema
Naye Msajili wa
Baraza la Wafamasia, Elizabeth Shekalage alisema kwa sasa wananchi wengi
wamechukulia huduma ya dawa ni biashara na kuwa baraza limejipanga kupambana na
watu wanaofanya huduma hiyo ni biashara huku wakikiuka maadili.
"Uchache wa
wanataaluma unasababisha kika mtu aone hii ni biashara huria na yeyote anaweza
kuifanya,kuna uhaba mkubwa wa fundi dawa sanifu,mafundi dawa wasaidizi,dawa ni
sumu hivyo tunasimamia hili ili kuepusha madhara kwa watumiaji"alisema Elizabeth
Kongamano la Mwaka
huu linaenda na kauli mbiu isemayo kuelezea ubora,usalama,ufanisi na
upatikanaji wa huduma bora za kifamasia.
Mwisho
No comments:
Post a Comment