PC Joseph Swai, enzi za uhai wake.
POLISI mkoani
Dodoma wanamsaka mkazi wa Chang’ombe Juu, Tisi Malya kwa kumuua askari
polisi kwa kumcharanga mapanga wakati akijaribu kumuokoa mtoto wa miezi
minane aliyekuwa anataka kuuawa na mtu huyo.
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Dodoma, David Misime amemtaja askari aliyeuawa jana majira
ya saa 5:00 asubuhi kuwa ni Joseph Swai.
Akisimulia mkasa huo
kwa waandishi wa habari, Kamanda Misime alisema kuwa askari huyo
aliitikia mwito uliofika kwake wa kuwepo kwa dalili ya tendo la jinai
nyumbani kwa mkazi mmoja wa Chang’ombe Juu katika Manispaa ya Dodoma.
Alisema
askari huyo alipigiwa simu na Mtendaji wa Mtaa wa Chang’ombe Juu,
akimjulisha kuwa amepokea taarifa ofisini kwake kutoka kwa Oliver
Baltazar (52) mkazi wa Chang’ombe Juu kuwa mtoto wake, Tisi Sirili
anaonekana anataka kumuua au ameshamuua mtoto wake wa miezi minane,
Valerian Tisi.
Alisema baada ya kupokea taarifa hiyo, askari
huyo alikwenda ofisini kwa mtendaji huyo ambapo waliongozana hadi
nyumbani kwa mtuhumiwa.
“Alipofika askari aligonga mlango huku
akijitambulisha kuwa yeye ni askari ili mtuhumiwa atoke nje, alichofanya
mtuhumiwa ni kumnyanyua mtoto wake mdogo wa miezi minane kwa mkono
mmoja kichwa chini miguu juu na kutaka kumkata kwa panga huku akisema,
‘namkata shingo na sitaki kuona mtu’.
“Askari aliamua kumwokoa
mtoto huyo kwa kumrukia mtuhumiwa, lakini kwa bahati mbaya aliteleza na
ndipo mtuhumiwa akamkata kichwani askari wetu,” alisema Misime.
Alisema
pamoja na askari huyo kuanguka, mtuhumiwa aliendelea kumkatakata kwa
panga huku mtendaji na kijana waliyekwenda naye eneo la tukio,
wakikimbia huku wakipiga kelele za kuomba msaada.
Alisema
mtuhumiwa baada ya kufanya kitendo hicho cha kin- yama, alikimbia akiwa
na panga lake huku nguo zake zikiwa zimetapakaa damu.
Aidha,
alisema katika hekaheka hizo, mama wa mtoto baada ya kuona mtoto
amebwagwa na askari ameanguka chini, naye alimkwapua mtoto na kukimbia
naye mahali pasipojulikana.
Alisema polisi wanamsaka baba huyo na mama huyo kwa ajili ya usalama wake.HABARILEO
No comments:
Post a Comment